Timu za michezo mbalimbali za TPDC zikiandamana kuingia uwanja wa michezo wa Chuo cha Ushirika ambao wafunguzi rasmi wa Michuano ya Mei Mosi umefanyika leo tarehe 22 Aprili, 2017.

Timu ya Mpira wa Miguu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania yazidi kujikita kileleni kwenye mashindano ya Mei Mosi yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro baada ya kuizamisha timu ya mpira wa miguu ya uchukuzi kwa jumla ya mabao 2-0.

TPDC imefanikiwa kupata ushindi huo kupitia wachezaji wake mahiri Phinias Ademba ambaye aliipatia timu yake gori la kwa kwanza mnamo dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza ambapo gori hilo lilidumu hadi kipindi cha pili dakika ya 58 pale mchezaji Walter Mwanga alipoipatia timu ya TPDC gori la pili lililodumu hadi mwisho wa mchezo.

Ushindi huu umeifanya TPDC kuongoza katika kundi kundi B ikiwa na jumla ya point sita na magori matatu ikifuatiwa na Hai DC ikiwa na pointi tatu. Katika mechi awali TPDC ilijipatia pointi tatu baada ya kuifunga timu ya Hai DC gori moja kwa sifuri. TPDC inatarajia kushuka dimbani tena tarehe 26 kuchuana na timu ya Mpira wa Miguu ya Moshi DC.
Wachezaji wa timu za michezo za TPDC wakila kiapo cha kuzingatia sharia za michezo na nidhamu mbele ya Mgeni rasmi wakati wa sherehe za ufunguzi wa Mashindano ya Mei Mosi.
Timu ya Kamba ya TPDC wakichuano vikali na wapinzani wao wa MUHAS (hawapo pichani) katika mashindano ya kuvuta kamba ambayo yamefanyika tarehe 22 Aprili, 2017.
Wachezaji wa TPDC wakitoka uwanjani kwa mbwembwe wakisindikizwa na wafanyakazi wenzao waliokuwa wakishuhudia timu yao ikitoa kipigo kikali dhidi ya Uchukuzi.
Baadhi ya watumishi wa TPDC wakishangilia na kuipongeza timu yao mara baada ya mechi dhidi ya TPDC na Uchukuzi kukamilika huku TPDC ikiibuka na ushindi wa magori 2-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...