THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RWANDAIR LOW FARES TO GREAT CITIESRAIS MAGUFULI AONDOKA UGANDA MARA BAADA YA KUHUDHURIA VIKAO VYA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC)

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa ndege wa Entebe mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambao ulimalizika hapo jana jijini Kampala nchini Uganda. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kijeshi kutoka Uganda kabla ya kurejea nchini. PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kijeshi kutoka Uganda kabla ya kurejea nchini. PICHA NA IKULU


RAIS MAGUFULI AREJEA NCHINI AKITOKEA NCHINI UGANDA ALIPOHUDHURIA MKUTANO WA 19 WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa MKoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) MKoa wa Mwanza ndugu Anthony Dialo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ndugu Kheri Jamesn mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akitazama ngoma mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa MKoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula,Mkuu wa MKoa wa Mwanza John Mongella na wacheza ngoma waliofika kumlaki uwanjani hapo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


PICHA NA IKULU.


KUNA WATU WANAJIDAI WANASHAHADA ZA UCHUMI KUMBE MAMBUMBU WA UCHUMI-Dk MPANGONa Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Philipo Mpango amesema kuna baadhi ya watu nchini wamekuwa wakijidai wana shahada za uchumi lakini kiuhalisia ni mambumbu wa uchumi.

Pia amesema kutungwa kwa sera au kufanyika kwa maamuzi yasiyoendana na taaluma ya uchumi kunakopelekea kuumiza wananchi masikini kutokana na uwepo wa wachumi feki ambao wanapewa nafasi serikalini ,vyuoni hata kwenye sekta binafsi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo na nyingine iko haja nchi kuwa na jJumuiya ya Wachumi au chama hai cha wachumi na chenye nguvu kwani ni muhimu sana.Dk.Mpango amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi chama cha Jumuiya ya Wachumi (EST) ambapo ametoa sababu tatu za umuhimu wa jumuiya hiyo.

Amefafanua sababu ya kwanza tasnia ya uchumi ina nafasi ya pekee katika kazi ya kujenga nchi kijamii,kiuchumi na hata kisiasa."Wachumi tunategemewa tuwe viongozi .Bila shaka waumini wenzangu wa John Maynard Keynes kuna maneno amewahi kuyasema na naomba nimnukuu.

Amesema hivi mawazo ya wachumi na wanafalsa wa siasa ,yawe sahihi au so sahihi yana nguvu kuliko inavyoeleweka kwa wengi."Watu wanaojiamini kwamba wako guru na ushawishi wa wanataaluma ,kiuhalisia watu hao ni watumwa wa mchumi fulani marehemu," amesema Dk.Mpango wakati ananukuu manneo ya Keynes.

Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji TIC na Mwenyekiti wa Kamati Uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wachumi Tanzania Economics Society Of Tanzania (EST) Bw. Godfrey Mwambe akipokea katiba ya Chama hicho kutoka kwa Vick Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT)kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa jumuiya hiyo kwenye ukumbi wa BOT leo jijini Dar es salaam, ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati anayeshuhudia ndiye aliyezinduam, Kulia ni Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati akizindua katiba ya chama hicho kwa kushirikiana na Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga na mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali wachumi wakishiriki katika zoezi hilo.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati pamoja na Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga na mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali wachumi wakionyesha katiba ya Jumuiya hiyo baada ya kuzinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam.


IDARA YA UHAMIAJI WAFANYA USAFI KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM, SHULE YA MSINGI MATUMAINI


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

IDARA ya Uhamiaji nchini imefanya usafi katika Kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu na Shule ya Msingi ya Matumaini ya Jeshi la Waokovu ‘Salvation Army’ iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kufanya usafi katika shule hiyo,kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Idara hiyo , Kamishina wa Utawala na Fedha, Edward Chogera amesema tangu kutangzwa Siku ya Jumamosi ni ya kufanya usafi Idara yai imekuwa ikifanya jitihada za kufanya usafi huo katika maeneo ambayo yana mchango kwa jamii.

Amesema shule ya Matumaini na kituo ni sehemu muhimu kutokana na watoto wanaosoma hapo kuwa na mahitaji maalumu.Kituo hicho hakiwezi kufanya chenyewe kutokana na mazingira ya watoto hao.Ameongeza mbali ya kufanya usafi katika kituo hicho wametoa pia msaada wenye thamani sh.500,000 ambao umetokana na wafanyakazi wa idara na wadau wenye ni njema kusaidia kundi maalumu ya kituo cha Jeshi la Uokovu .

Aidha amesema katika kipindi kijacho wamepanga kuwafikia watu wengine katika kufanya usafi ikiwa ni sehemu ya wafanyakazi kujua jamii inayowazunguka.Msaada waliotoa ni , Mchele, Maharage sukari , Mafuta ya kula , Sabuni za kuogea , Unga wa mahindi na mafuta ya kupakaa kwa wanafunzi wenye Ualbino .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho,Timoth Sinana amesema licha kupata elimu,watoto wamekuwa wamekuwa wakiendelezwa kwenye mambo mbalimbali yakiwamo ufundi nguo na kuendeleza vipaji vyao.Amesema wanafunzi hao wamekuwa bora kimkoa katika suala la vipaji.
Kamishina wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji , Edward Chogera akizungumza wanafunzi na walimu pamoja na walezi wa kituo na shule ya Matumaini ya Jeshi la Waokovu Salvation Army mara baada ya kumaliza usafi katika kituo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha Jeshi la Waokovu pamoja shule ya Matumaini, Timoth Sinana akizungumza kuhusiana na historia ya shule hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1969 pamoja na mafanikio ya shule hiyo .
Msaada uliotolewa katika kituoa hicho ni , Mchele, Maharage sukari , Mafuta ya Kula , Sabuni za Kuogea , Unga wa Mahindi pamoja na mafuta ya kupakaa kwa wanafunzi Wenye Ualbino .  

Baadhi wa wafanyakazi katika shule ya msingi ya matumaini na kituo cha jeshi la Waokovu


FIFA KUONGEZA FEDHA ZA MAENDELEO NA KUJIENDESHA KWA SHIRIKISHO

Na Anitha Jonas –WHUSM

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuendeleza viwanja tisa nchini kufuatia kuongezeka kwa dau la pesa za Maendeleo na Kujiendesha zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA kuanzia mwaka 2019 .

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyojadili na Rais wa FIFA Gianni Infantino alipokuwa nchini kwa mkutano wake hivi karibuni.

‘’Rais wa FIFA alieleza kuongeza mara nne ya kiwango cha pesa za maendeleo na kujiendesha walizokuwa wanatoa kwa mashirikisho kama TFF mpaka kufikia Dola Milioni Moja na Laki Mbili na Nusu kwa mwaka na kusema pesa hizo ndiyo zitumike kuendeleza viwanja vya michezo kwani uwepo wa viwanja ndio unaosaidia kukuza vipaji vya soka,’’alisema Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa Rais huyo wa FIFA ametoa msisitizo wa kutokuwa na huruma kwa kiongozi yoyote wa shirikisho atakayekuwa na matumizi mabaya ya pesa pamoja na kufanya udanganyifu kwani yeye yuko mstari wa mbele kupinga ufisadi katika sekta ya maendeleo ya Soka duniani.

Pamoja na hayo nae Rais wa TFF Bw. Wallace Karia alitoa ufafanuzi wa hali ya kifedha kwa shirikisho na kueleza kufuatia kuwepo na matatizo katika shirikisho hilo FIFA ilikuwa imesitisha kuwapatia fedha hizo za maendeleo na kujiendesha tangu mwaka 2015 lakini baada ya kuingia uongozi mpya ambao FIFA wameridhika nao na wameshaupa utaratibu wa kufuatilia fedha hizo.

‘’Rais wa FIFA alitueleza kuwa fedha hizo ziko salama nchini Zurich ni kwamba tu hazikuwa zimeruhusiwa kuingia nchini na kwa sasa tumeshaanza mchakato wa kufuatilia fedha hizo kwa kuzingatia maelekezo ya FIFA hivyo basi tutakapo pata fedha hizo Shirikisho litaendeleza baadhi ya miradi ambayo tumekwisha iandaa,’’alisema Bw. Karia.

Pamoja na hayo rais huyo alitoa wito wa wakazi wa jiji la Tanga waliyovamia eneo linalotarajia kujengwa Technical Center ya mchezo wa soka basi waondoke mara moja kabla hawajachukuliwa hatua.
Waziri Wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyozungumza na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino na Rais wa CAF Ahmad Ahamad alipokuwa nchini kwa ajili ya mkutano wao leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu hali ya kifedha kwa shirikisho hilo na matarajio baada ya FIFA kuwapa maelekezo ya kufuatilia fedha ambazo hawakuingiziwa kutokana na matatizo ya viongozi waliyopita leo jijini Dar es Salaam.


MBUNGE VITI MAALUM RUVUMA AWAPIGA TAFU WAKULIMA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Mh.Jacqueline Ngonyani Msongozi ametoa mkopo wa Mbolea kwa vikundi vya akinamama na Vijana vipatavyo 75 vyenye wanachama wapatao 1030 mkoani Ruvuma. Mkopo wa Mbolea wenye masharti nafuu tani 151.05 zenye thamani ya TZS 129,124,500 .


DK.KAMANI AWAONYA VIONGOZI VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI

Na Said Nwishehe,Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dk.Titus Kamani amesema Serikali kupitia tume hiyo ni awaelekeza viongozi wa Vyama vya Ushirika kutojihusisha kuuza mali za vyama hivyo pasipo kuzingatia sheria.

Hivyo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuuza mali za vyama hivyo na kufafanua ili kudhibiti hali hiyo Ofisi za Mrajisi wa vyama vya ushirika imekuwa ikichukua hatua ikiwa pamoja na kuwaondoa viongozi wanaokiuka sheria.

Dk.Kamani amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anaelezea udhibito wa mali za ushirika na mpango wa makusanyo na mauzo ya mazao makuu matano ya kimkakati kupitia mfumo wa ushirika.

Amesema vyama vya ushirika nchini vinaendeshwa kwa kuzingatia sheria ya vyama vya ushirika namba 6 ya mwaka 2013.Hivyo vyama vinapaswa kuzingatia sheria wanapotekeleza majukumu yao.Dk.Kamani amesema Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika inaelekeza viongozi wa vyama hivyo kuwa makini kuzingatia sheria.

Amefafanua vyama vina haki ya kumiliki mali na kuuza mali hizo pale itakapoona inafaa kwa kuzingatia shetia iliyopo.Pia mali zinazomilikiwa na vyama zinapaswa kuwa zimerasimishwa ili kuleta uhalali wa umiliki.


DK MWANJELWA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA, ATETA NA KINA MAMA WANAOJITEGEMEA 'SINGLE MOTHERS'

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea machache na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza alipofika kwa utambulisho na kuanza ziara katika Mkoa huo Februari 23 2018. Pamoja naye (kushoto) Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga viongozi wa wasaidizi wake mkoani humo.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akisalimiana na mmoja wa wageni alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kulia) alipofika kwa utambulisho na kuanza ziara katika Mkoa huo Februari 23 2018. Kulia kwa Naibu Waziri ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga. 
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiagana na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Amina Masenza baada ya kufanya naye mazungumzo ofisini wakati wa kuanza kwa ziara yake mkoani humo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akikagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Katikati ni mwenyeji wao, Mhe Amina Masenza Mkuu wa Mkoa.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akibadilishana mawazo na wakina mama wanajitegemea 'Single mothers' baada ya kukagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 mkoani Iringa kwa ajili ya kilimo cha biashara maalum kwa ajili yao, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za awali na Msingi. 


MEYA JIJI LA DAR AWASILISHA MPANGO WA BAJETI BIL 75.2/- ,MADIWANI WAUPITISHA

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii 

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita amewasilisha mpango wa Bajeti wa mwaka 2018 hadi 2019 ambapo jumla ya Sh. bilioni 75.2 zitatumika kwa mwaka huo katika shughuli mbalimbali.

Baada ya kuuwasilisha mpango huo kwenye Baraza la Madiwani umepitishwa kwa kauli moja na madiwani hao huku wakipongeza kuwa Jiji la Dar es Salaam limepata Meya anayejali maslahi ya wananchi wa Jiji hilo.

Akizungumza alipokuwa akiwasilisha Mpango huo wa bajeti,Mwita amesema Halmashauri hiyo imeandaa mpango huo kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa kufuatwa na mamlaka za Serikali za mitaa katika utayarishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha wa 2018 na 2019.

Amefafanua Jiji linatarajia kukusanya na kutumia Sh. bilioni 75.2 itakayotokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo Sh.bilioni 18.1 ambazo zinatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye vyanzo vya vyandani.

"Mapato mengine yatapatikana kutokana na halmashauri kubuni vyanzo vingine vya mapato sambamba na kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa mapato." Utekelezaji wa bajeti hiyo umelenga kutekelaza mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis,kuboresha miundombinu ya Dampo,ujenzi wa vyoo vya Umma na kuhakikisha utoaji wa huduma usiokua na usumbufu kwa wananchi,"amesema Mwita.

Ameongeza Jiji la Dar es Salaam limepanga kutumia asilimia 65 ya mapato ya ndani sawa na Sh.bilioni 11.7 kwa ajili ya kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo huku Sh. bilioni 1.08 zitatumika kwa ajili ya mfuko wa wanawake ,vijana na wal

Kuhusu utalii,Mwita amesema kwenye bajeti hiyo zaidi ya Sh.bilioni mbili zimetengwa kuboresha sekta ya hiyo ikiwemo kununua mabasi ,kutengeneza na kuboresha vivutio mbalimbali vilipo jijini hapa.


TAARIFA YA KUSITISHA MATUMIZI YA ADA MPYA KWA WAANDAAJI WA MBIO ZA MARATHON

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limepokea tamko la Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kuhusu mada tajwa hapo juu Februari 20, 2018 kwa barua yenye Kumbukumbu namba: BMT/A/2/Vol. 18/69, pia kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

BMT imeagiza kusitishwa ada hizo hadi Machi 5 itakapotoa maelekezo mengine baada ya kukutana na RT na waandaaji.

Sisi RT tumefedheheshwa na uamuzi huo na jinsi njia iliyotumiwa na BMT katika kulishughulikia tatizo linalodaiwa kuwa malalamiko ya waandaaji wa marathon kudai kuwa tozo hizo ni kubwa, tofauti na wanachokiandaa au kukifanya.

Kwani tuliamini, kutokana na miongozo ya kiutendaji, BMT ingekuwa mstari wa kwanza kulinda matakwa ya Katiba ya RT kiutendaji.

Tuliamini BMT inajua mamlaka ya utendaji ya RT, hivyo kabla ya kufikia uamuzi huo, ingetuita RT kwanza na kujadili hicho kinachodaiwa kuwa malalamiko, ndipo ingefikia kuanza kuchukua hatua.

KUPANDISHWA ADA;

Kutokana na mwenendo usioridhisha kwa muda mrefu kuhusu uandaaji wa mbio za Marathon kiholela, ambao ulikuwa haufuati taratibu zinazotakiwa, hata BMT yenyewe ni shahidi kutokana na matamshi mbalimbali ya Watendaji wake, RT iliamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Katiba yake kama msimamizi mkuu wa mchezo wa Riadha nchini.

Mnamo Septemba 16, 2017 RT ilitoa mwito kwa waandaaji wa mbio za Marathon na kukutana katika moja ya kumbi za Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambako takribani waandaaji 28 - 30 walijitokeza.

Katika kikao hicho ambacho kilikuwa cha wazi na huru, RT iliwaeleza waandaaji kuhusiana na utaratibu mzima wa uandaaji wa mbio za Marathon na utaratibu mpya unaotakiwa kuanza kutumika kuanzia January 2018, ikiwamo kujisajili na kuzitenga mbio hizo katika makundi manne ya A, B, C na D kulingana na ukubwa wa mbio husika na kila kundi na gharama zake.


OSHA YASISITIZA KADA YA USALAMA KAZINI KUTAMBULIKA RASMI


Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) unakusudia kuishawishi serikali na waajiri katika sekta binafsi hapa nchini kuitambua kada ya Usalama na Afya mahali pa kazi na kuiweka katika mfumo rasmi wa ajira.

Mpango huo uliwekwa wazi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi.Khadija Mwenda, alipowahutubia wahitimu wa Kozi ya Taifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi katika hafla ya kufunga kozi hiyo Februari 23,2018 jijini Dar es salaam. Kozi hiyo pamoja na nyingine zinazohusu Usalama na Afya kazini hutolewa na Wakala huo wa serikali.

Mtendaji Mkuu huyo alisema kwasasa kada ya maofisa Usalama Mahali pa Kazi (Safety Officers) bado haitambuliki katika mfumo rasmi wa ajira hapa nchini jambo linalopunguza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.

”Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003, inawataka waajiri kuunda Kamati za Usalama na Afya katika sehemu zao za kazi ambazo wajumbe wake ni wawakilishi wa wafanyakazi ambao kimsingi wana majukumu yao mengine tofauti na kusimamia masuala ya usalama na afya mahali pa kazi. Hivyo jukumu la kusimamia usalama na afya wa wafanyakazi wenzao katika sehemu za kazi husika linakuwa ni la ziada,” alisema Bi. Mwenda.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akiwahutubia wahitimu wa Kozi ya Taifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu wa OSHA, Bw. Joshua Matiko, akiongea na wahitimu wa Kozi ya Taifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Kozi ya Taifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, wakati wa hafla ya kufunga kozi hiyo iliyofanyika katika ofisi za Wakala jijini Dar es Salaam.


KIGWANGALLA ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA, ATUMA SALAMU KWA MUWEKEZAJI ANAECHOCHEA MGOGORO KATIKA HIFADHI HIYO


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Martin Loibooki na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga (kulia).  
Waziri wa Malisili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA, Martin Loibooki kuhusu Kreta ya Hifadhi ya Ziwa Manyara muda mfupi kabla ya kuhitimisha ziara yake katika hifadhi hiyo jana jioni. (Picha na Hamza Temba-WMU).


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


MPINA AZIPIGA FAINI MELI 19 ZILIZOTOROKA BILA KUKAGULIWA

Na John Mapepele

Serikali imezipiga faini ya bilioni kumi na tisa meli 19 ikiwa ni shilingi bilioni moja kwa kila meli na kuamuliwa kulipa faini hiyo ndani ya wiki mbili kwa kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kutoripoti katika bandari Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara ama Tanga kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutoka katika bahari kuu ya Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, katika Ofisi za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu zilizopo Fumba kisiwani Unguja, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina amesema pamoja na meli hizo kuamriwa kulipa faini ya Shillingi Billioni moja (Tshs. 1,000,000,000) kila moja zinatakiwa kurejea katika bandari za Tanzania kwa ajili ya ukaguzi kwa kuwa leseni zao bado hazijaisha muda wake hadi sasa ili kubaini thamani halisi ya kiasi cha fedha zitakazotozwa kwa ajili ya samaki waliovuliwa bila kukusudia(Bycatch).

Aidha Mpina amesema meli hizi zimetakiwa kuilipa Tanzania kiwango cha pesa kwa mujibu wa soko la kimataifa kutokana na kuondoka na Bycatch waliyoripoti kuwa wanayo kabla ya kutoroka.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu)akimsikiliza Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed ofisini kwake leo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Kisiwa Unguja. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlakaya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA),Hosea Gonza Mbilinyi. (Picha na John Mapepele)
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) na kulia kwake ni Katibu Mkuu Uvuvi Tanzania Bara Dkt. Yohana Budeba wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na Watendaji wa Sekta ya Uvuvi mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John Mapepele)
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA) wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina  (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo katika ofisi ya Mamlaka hiyo Fumba katika kisiwa cha Unguja leo. 
Kiongozi wa Kampuni ya Linghang kutoka china inayoshughulika na uendelezaji wa Utalii wa Zanzibar nchini china Tom Zhang (katikati) akiwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John Mapepele).MICHUZI TV: Mlezi Wa Ukonga Jogging Club Bi Rahel Martin Emil azikwa Kisarawe Mkoa Wa Pwani leo


RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA AFRIKA MASHARIKI

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Rais wa Uganda Yoweri Museveni pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo katika siku ya mwisho ya Kikao chao kilichofanyika Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anatoka katika ukumbi wa mkutano pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC vilivyofanyika Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa EAC katika siku ya mwisho jijini Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU


RC Wangabo Asisitiza Kutumia Bidhaa Za Viwanda Vya Ndani Kujihakikishia Soko


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa na watanzania kwa ujumla kujenga mazoea ya kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyopo kwenye maeneo yao ili kujihakikishia soko la ndani na hatimae kuvuka mipaka ya nchi.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea Kiwanda cha Unga Energy Sembe na Kiwanda cha maji Dew Drop vinachomilikiwa na Azizi Mohamed Sudi, Mbasira Fodd Industries na Kiwanda cha maziwa OTC Kizwite kinachomilikiwa na kikundi cha wafugaji vyote vikipatikana katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa vinavyozalisha bidhaa zinazouzwa ndani ya Mkoa, nje ya Mkoa na kuvuka mipaka ya nchi.

Amesema kuwa Kazi ya Serikali kutoa mazingira bora na wezeshi ili wawekezaji wawe na fursa nzuri za kuwekeza na kuongeza kuwa serikali haitakubali kuona viwanda vikifa kwa mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa serikali na kuwahakikishia wamiliki wa viwanda hao kuwa serikali haiwezi kuendelea kuhamasisha viwanda bila ya kutatua changamoto mbalimbali zinazokumba viwanda vilivyopo.

“Tujivunie viwanda vyetu vya hapa, hasa vile vinavyozalishwa na wazawa wenyewe ambavyo vinatoa ajira kwa wananchi wa Mkoa huu, changamoto zipo kama masuala ya kimazingira, malighafi na umeme, kama serikali tutayachukua ili kuhakikisha wawekezaji wanafanya kazi katika mazingira bora kabisa, kazi ya serikali kuweka mazingira wezeshi ili wenzetu waweke viwanda ili tuweze kufikia uchumi wa kati wa Viwanda kufikia 2025,” Alisema.

Na kushauri kuwa viwanda hivyo havinabudi kujitangaza katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ili kuweza kupata masoko ya uhakika.Kwa upande wake Mmiliki wa Kiwanda cha Unga Energy Sembe na Dew Drop, Aziz Mohamed Sudi amesema kuwa kiwanda cha sembe kimesimama uzalishaji wake tangu Mei, 2017 baada ya kukosa soko la ndani ya nchi na kutegemewa kuanza tena mwaka 2018 baada ya kupata maombi kutoka nchi ya Kongo.

“Wawekezaji katika mikoa ya pembezoni tumekuwa mbali na masoko makubwa, gharama za uzalishaji, umeme na kupeleka bidhaa hizo kwenye masoko makubwa zimekuwa kubwa pamoja na pamoja na utititiri wa kodi, hivyo tunaiomba serikali iruhusu kuuza bidhaa za kiloimo zilizoongezwa thamani na tunakubalina na hatua za kudhibiti chakula kwa kuuza nafaka,” Azizi Alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akionyeshwa baadhi ya Vichachuzi na Mwenyekiti wa Kikundi cha Wafugaji wanaomiliki Kiwanda cha maziwa Paulo Malongo, wakati alipotembelea kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchakata lita 1000 za maziwa kwa siku.
Mmiliki wa Kiwanda cha Dew Drop Azizi Sudi akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo virutubisho vilivyomo ndani ya maji yaliyotengezwa kwenye kiwanda hicho .
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili kutoka kushoto) akiwa ameongozana na Mmiliki wa Kiwanda cha Dew Drop Azizi Sudi (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule walipotembelea kiwanda hicho. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyeshika ungo) akiangalia ubora wa mahindi kabla ya kuwa unga alipotembelea kiwanda cha Mbasira Food Industries Ltd.