Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema nia ya Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India wa kuonyesha muelekeo wa kutaka kuwekeza miradi yao katika sekta ya Kilimo utaleta matumaini makubwa ya kuimarika kwa Uchumi Visiwani Zanzibar. 
Alisema hatua hiyo itafungua milango ya Uwekezaji kwa Taasisi na Makampuni ya Uwekezaji ya Jimbo la Kerala Nchini India kuanzisha miradi yao Zanzibar hasa ikizingatiwa kwamba Utamaduni pamoja na mazingira ya pande hizo mbili yanafanana. 
Balozi Seif Ali Iddi akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wawili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwanzo wa ziara yake ya Wiki Moja Nchini India alitoa Kauli hiyo wakati wa Kikao cha pamoja kati ya ujumbe wake na Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India {CII} hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Kimataifa ya Crowne Plaza Mjini Kochi katika Jimbo la Kerala. 

 Ujumbe wa Serikali ya Zanzibnar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Kulia ukifanya mazungumzo na Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India {CII} hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Crowne Plaza Mjini Kochi Jimboni Kerala India.

Balozi Seif wa Pili kutoka Kulia akiuongoza Ujumbe wa Zanzibar katika Mkutano na Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India. Wa kwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini India Balozi Mohamed Hija, Kulia ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiye na Wizara Maalum Dr. Sira Ubwa Mamboya na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Nd. Juma Ali Juma akitoa ufafanuzi wa Mikakati ya Zanzibar katika uimarishaji wa fursa za uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo na Uvuvi kwa Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India. Kushoto ya Ndugu Juma ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini India Bibi Haika Msuya na Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd.Abdulla Hassan Abdulla {Mitawi }.
Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Waziri asiye na Wizara Maalum Dr. Sira Ubwa Mamboya akitoa uzoefu wake katika sekta ya Kilimo kwa Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India ambao haupo pichani.
Balozi Seif  wa nne kutoka kushoto waliokaa vitini na Ujumbe wake akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India mara baada ya kumaliza kikao chao cha ushirikiano. Kushoto ya Balozi Seif  ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini India Bwana  George Paul. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...