Na.Aron Msigwa- Dar es salaam.

Wito umetolewa kwa Taasisi,mashirika, makampuni na watu binafsi kuanzia ngazi ya familia kuendelea kuitumia Siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kufanya usafi wa mazingira, kupanda miti na kutunza vyanzo vya maji kwa hiari bila kusubiri kushurutishwa na sheria kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wakiwemo wafanyabiashara na wafanyakazi wa taasisi na mashirika mbalimbali waliokuwa wakitekeleza wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam leo wamesema kuwa hatua ya Serikali kuirasimisha Siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi wa mazingira kitaifa inaweka msisitizo kuhusu jukumu la kila mwananchi kuwa mlinzi na mwangalizi wa mazingira katika sehemu anayoishi.

Wamesema Suala la usafi wa mazingira linawahusu watu wote, hivyo kila mwananchi anao wajibu wa kushiriki kikamilifu kufanya Usafi wa Mazingira kwenye Makazi yake, Maeneo ya Biashara, maeneo ya Taasisi za Umma na maeneo yenye mikusanyiko ya watu mbalimbali kama masoko na minada.

Bi. Zaituni Musa mkazi wa Mwananyamala, Kinondoni jijini Dar es salaam aliyekuwa akisafisha mifereji eneo la mtaa anaoishi akishirikiana na wananchi wenzake amesema kuwa suala la usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi bila kuangalia cheo au nafasi yake katika jamii kwa kuwa kuishi katika mazingira machafu kuna athari kubwa kiafya hususan kuchangia milipuko ya magonjwa ikiwemo Kipindupindu.

" Suala la usafi wa mazingira linatuhusu sote, ni wakati wa kuchukua hatua na kuacha kuishi kwa mazoea,nawaomba watanzania wenzangu tufanye usafi bila kulazimishwa na Serikali kila mmoja atimize wajibu wake" Amesisitiza Bi.Zaituni.


Baadhi ya Wafanyakazi wa DAWASA waliokutwa wakifanya usafi wa mazingira kutii agizo la Kufanya Usafi kwa kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi ili kuyaweka maeneo ya Ofisi za Malamka hiyo katika hali ya usafi.

Baadhi ya Wakazi wa Mwananyamala wakipakia Taka walizozoa katika mitaa yao katika gari la kuzoa Taka la Manispaa ya Kinondoni.

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi wa Mazingira katika maeneo mbalimbali, Mwananyamala jijini Dar es salaam.

Baadhi ya Wafanyakazi wa DAWASA waliokutwa wakifanya usafi wa mazingira kutii agizo la Kufanya Usafi kwa kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi ili kuyaweka maeneo ya Ofisi za Malamka hiyo katika hali ya usafi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...