THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.
THANKS GIVING DINNER @ SAFARI DC FOR $10 FROM 5 -11 PM THEN PARTY TILL 2AM

**WE SAY THANKS FOR SUPPORTING US **

ORDER CHAKULA CHOCHOTE KWENYE MENU KWA $10 TU 
HALAFU PARTY HADI SAA NANE USIKU


WANAVYUO DODOMA WAASWA KUJALI NAFASI WALIYONAYO

 Kwaya ya pamoja inayojumuisha Vyuo vikuu vyote vya Dodoma (Mass Choir) ikiimba wimbo maalum kwenye mkesha wa kusifu na kuabudu uliosema ‘Dodoma izidi kung’ara’ ikiwa ni sehemu ya maombi yao kwa mkoa huo
    Kwaya ya New Life Band ya Arusha ikitoa burudani ya kuimba kwa bass bila ala za muziki kwenye mkesha wa kusifu na kuabudu (Campus Night) uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Chimwaga, mjini Dodoma. 
Kwaya ya Abednego & The Worshippers ya Arusha ikitoa burudani kwenye mkesha wa kusifu na kuabudu (Campus Night) uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Chimwaga, mjini Dodoma. Picha zote na habari na Irene Bwire
 MKUU wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu vya mkoa wa Dodoma watumie fursa waliyonayo kuisaidia nchi ya Tanzania isonge mbele na kufikia uchumi wa juu zaidi. 
 Alitoa nasaha hizo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanavyuo hao kwenye ukumbi wa Chimwaga, Dodoma wakati wa mkesha wa kusifu na kuabudu (Dodoma Campus Night) ulioandaliwa maalum kwa ajili ya kuwajenga kimaadili wanafunzi wa vyuo vya mkoa huo.
 Dk. Nchimbi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa Njombe, aliwaasa wanafunzi hao waache kuendekeza matumizi ya simu za mkononi kwa kutumiana meseji ambazo zinawatoa kwenye umakini wa masomo yao.
 “Inasikitisha kuona mwanafunzi akiingia mwaka wa kwanza anakuwa mwema, lakini baada ya muda anarudi nyuma kimaendeleo… kisa meseji anazotumiwa”. “Muwe makini na masomo yenu. Angalieni mavazi yenu, angalieni mienendo yenu, jichungeni msiyumbishwe na tabia za makundi lakini kikubwa zaidi ni kutambua nafasi mlizonazo na kusimama imara ili kuisadia nchi hii isonge mbele na kufikia uchumi wa juu zaidi,” alisema. 
 Mapema, akimkaribisha kuzungumza na wanafunzi hao, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG-ICC Dodoma, Dk. Gerald Ole Nguyaine aliwaambia wanavyuo kwamba wanapaswa kuiheshimu nafasi hiyo ya pekee ambayo Mungu amewapa. 
 “Hebu jiulize ni wanafunzi wangapi ambao wamebaki huko nje na wanatamani kuingia Chuo Kikuu… ni lazima muwe focused ili kuitendea haki nafasi mliyoipata. Na kama unataka kuwa mtu ambaye Mungu alikusudia uwe, ni lazima ujisalimishe kwake,” alisema.
Akitoa mafundisho kwa wanavyuo hao, Mchungaji Casey Kalaso wa Kanisa la Utume wa Kristo kutoka Kabwe, Zambia aliwataka wanavyuo hao watambue kuwa mafanikio yanakuja pale mtu anapofanya maandalizi na kutumia vizuri fursa aliyonayo. 
 “Changamoto kuwa inayotukabili hivi sasa ni kwa mwanadamu kutojua majira aliyomo… watu wengi hatujui nini tunapaswa kufanya na kwa wakati gani. Usipokuwa mwangalifu utalia baadaye wakati ulichezea fursa uliyoipata sasa,” alisema. 
 Akitumia mfano wa Samson na Delila kutoka kitabu cha Waamuzi (sura ya 13), aliwataka waithamini nafasi waliyonayo kwani ikipotea ni nadra kuipata tena na kuitumia vizuri. 
 “Usiangalie mambo ya nyuma, angalia nafasi ya sasa unayopewa na Mungu na uifanyie kazi. Jihadhari na watu wanaokuja maisha mwako, wako wanaokuja kukuongezea thamani lakini wengine wanakuja ili kukufanya uwe dhaifu zaidi,” aliwaonya. 
 Naye Mchungaji Mathew Sasali wa Kanisa la TAG Mbeya aliwataka wanavyuo hao wajitambue nafsi zao na kubaini ni picha gani ambazo zimechorwa maishani mwao kama kweli wanataka kusonga mbele maishani mwao. 
 “Kuna watu waliambiwa hutafaulu kwa sababu katika ukoo wenu hakuna msomi, au fulani hutaolewa kwa sababu katika familia yenu hakuna aliyewahi kuolewa. Hizo zote ni picha zinazochorwa kwenye maisha ya watu na kuwazuia kufikia malengo wanayotamani kuyapata maishani mwao,” alisema. 
 “Kama hujagundua kuwa kuna picha imechorwa maishani mwako ni lazima tu itakutesa. Hiyo picha inatabiri ni vita ya aina gani unapigana nayo. Na usipoifuta hiyo picha, huwezi kutoka kwenye maisha uliyonayo… iwe ni ulevi, uzinzi, uvivu, na kadhalika,” alisema. 
 Alisema njia pekee ni kuibadilisha na kupambana na picha iliyowekwa mbele ya maisha yao. “Picha iliyo mbele yako siyo ile ambayo Mungu ameileta mbele yako. Taifa la Israel lisingeweza kwenda mbele kama picha nyingine isingechorwa mbele yao ambayo ilibadilishwa na Yoshua na Kaleb,” alisisitiza. 
" Ninawasihi tuchane picha zilizoletwa mbele yetu, iwe na ndugu, marafiki, wanaukoo au wachawi. Tuchukue hatua na kuikataa picha iliyo mbele yetu ambayo iko nje ya mpango wa Mungu. Fahamu zetu zikifunguka na kuiona picha ya Mungu, ndipo tutaanza kuchanua na kufanikiwa,” alisema. 
 Katika Campus Night hiyo ambayo ilihudhuriwa na wanavyuo zaidi ya 5,000, yalifanyika pia maombi kwa ajili ya vijana wote wa Tanzania, uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi Mkuu wa 2015 pamoja na mchakato wa Katiba Inayopendekezwa. 
 Wanavyuo hao wa dini mbalimbali wanatoka vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM), St. John’s, Vyuo vya Mipango, Madini, Mirembe, Hombolo, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na vyuo vya ualimu vya Mitumba na Capital.


Kijana Suleiman Othuman wa Zanzibar anaomba msaada wenu

Pichani kiijana Suleiman Othuman akiwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12. 

 Assalam Aleikum ndugu zangu mnaotusoma kwenye blog hii kila siku, msaada unahitajika kwa kijana Suleiman Othman Ally mwenye umri wa miaka 19, mkaazi wa Zanzibar, amepatwa na tatizo la uvimbe mkubwa kwenye mgongo wake baada ya kupatwa na ajali  kugongwa na Vespa kwa muda wa siku nyingi tu.
Walimpeleka Hospitali ya Mnazi mmoja ambapo ilishindikana kupata matibabu kutokana na damu nyingi aliotoka wakati wa upasuaji, hivyo kuwalazimu kumshona bila ya kumfanyia operation iliyokuwa wamemkusudia.
Kijana Suleiman Othuman hali yake inazidi kudhoofika na maumivu makali alionayo kwa sasa hawezi kukaa kusimama vizuri na hata kulala inavyostahiki kwa sababu ya ule uvimbe aliokuwa nao kwenye kiuno chake kam picha inavyojionyesha.
Hivi sasa familia yake haina budi kuomba ushirikiano wa msaada wenu kwa ajili ya kuweza kumpeleka nchini India kwaajili ya matibabu na kumgharamikia mtu wa kufuatana nae katika familia, kutokana na gharama ni kubwa na uwezo ni mdogo.
Hivi sasa yuko hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12.
Ndugu zangu tujitahidini kuokoa maisha ya ndugu yetu Suleiman Othuman kwa hali na mali.
Kwa mtu yoyote atakayeguswa na habari hii, na mwenye kutaka kuchangia msaada wake anaweza kuwasiliana na Mama yake mkubwa. Bi Salma.
Numba yaze za simu ni-:
 255777489015
Tigo: 255655489015
Pia unaweza kuwasiliana na Mdau wa Blog ya  
Abou Shatry Number 301-278, 3977, Email swahilivilla@gmail.com


Milla Sports Club a.k.a. Berlin ya Temeke yakabidhiwa vifaa vya michezo

 Timu ya Milla Sports Club ya Temeke maarufu kama Berlin imeadhimisha siku yake ya Milla Day katika hafla ambayo pia walikabidhiwa  vifaa vya michezo Jersey na mipira ili kusaidia timu hiyo iweze kushiriki ligi ya soka Wilaya ya Temeke. Timu hii ya Berlin imezalisha wanamichezo na viongozi wengi maarufu wa soka nchini. Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo MJUMBE wa NEC Ndg. Phares Magesa akitoa msaada huo wa vifaa vya michezo


VIONGOZI WA SUDANI KUSINI WAMFUATA KOMREDI KINANA MASASI KUPATANISHWA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinyanyua mikono juu kuashiria mshikamano na baadhi ya viongozi wa makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan Kusini ambao wako kwenye mgogoro wa kugombea madaraka kwa takribani mwaka sasa. Kinana amekutana na viongozi hao wakati wa mkutano wa hadhara mjini Masasi, Mtwara baada ya kumfuata kutaka ushauri wa upatanishi kutoka kwao Sudani Kuzini. Baada ya ya viongozi hao kupata wasaa wa kusalimia wananchi katika mkutano huo alifanya nao mazungumzo Ikulu Ndogo ya Masasi. 
 Kinana akiwa katika mkutano wa kuwapatanisha viongozi hao, usiku huu Ikulu Ndogo ya Masasi, Mtwara


introducing ngoma mpya ya lady jaydee 'forever'


SHILOLE ATUA UBELGIJI, IJUMAA KUFANYA SHOW LEUVEN NA JUMAMOSI BRUSSEL

 Furaha ilishika nafasi pale mwanadada shilole alipowasili uwanja wa kimataifa wa ndege wa Zaventem jijini Brussel.
 Msanii Shilole akiwa na furaha baada ya kupokelewa na wenyeji wake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem jijini Brussel.
The Big Boss Mohammed akiwa na msanii Shilole muda mfupi tu baada ya kuwasili uwanjani Brussel. Picha zaidi BOFYA HAPA


WANAFUNZI WA KITANZANIA WUHAN CHINA WASHIRIKI MAONESHO YA UTAMADUNI

 TAREHE 22 NOVEMBER 2014 UMOJA WA WANAFUNZI WA KITANZANIA WANAOSOMA JIJINI WUHAN CHINA (WUHAN TANZANIAN STUDENTS ASSOCIATION) ULIWAONGOZA WATANZANIA WANAOISHI JIJINI HUMO,KATIKA KUITANGAZA NCHI YA TANZANIA KATIKA MAONESHO HAYO YA KITAMADUNI YALIYOANDALIWA NA CHUO KIKUU CHA WUHAN(WUHANI UNIVERSITY) NA KUSHIRIKISHA MATAIFA MBALIMBALI YA AFRIKA,ULAYA ,AMERIKA YA KUSINI,AMERIKA YA KASKAZINI NA ASIA.
AMBAPO WUTASA ILITUMIA FURSA HIYO KUITANGAZA TANZANIA IKIWEMO MBUGA ZA WANYAMA,VYAKULA VYA KITANZANIA,MUZIKI NA MAVAZI PIA.
  MWANA MAMA WA KICHINA NA MWANAYE WAKIWA WANASUBIRI MUDA WA KUPATA HUDUMA UANZE.
 KATBU MKUU WA WUTASA(KULIA) NDUGU HASSAN MKOKO NA NDUGU NOEL ERNEST WAKIWA WANATOA HUDUMA KWA WAGENI WALIOTEMBELEA BANDA LA TANZANIA 
 WAGENI WAKIPATA HUDUMA KATIKA BANDA LA TA NZANIA
 SEHEMU YA MAELFU YA WATU WALIOKUWEPO KWENYE MAONESHO
 WAGENI WAKIENDELEA KUPATA HUDUMA KWENYE BANDA LA TANZANIA 
 HATA VYAKULA VYA KITANZANIA NAVYO VILIKUWEPO. HAPA WAGENI WAKIJIPATIA MLO WAO WA MCHANA WA KITANZANIA
 MHASIBU WA WUTASA ELVIS MULOKOZI AKIWA ANATOA HUDUMA KWA WAGENI,HUKU MWANADADA MARY NAFTALI AKIWA UPANDE WA KUGAWA MSOSI(CHAKULA CHA KITANZANIA 
BAADHI YA WANAFUNZI WA KITANZANIA KWENYE MAONESHO HAYO


NBC Bank and MTT Ltd signs a preferred Supplier Agreement deal.


The NBC Head of Corporate and Investment Banking, Theobald Sabi (left) signs documents with Executive Director for MTT Limited which is the sole authorised dealer of JCB products in Tanzania, Mr Andrew Fimister (right) at an event where the two signed Preferred Supplier Agreement on behalf of their two organisations in Dar es Salaam on Friday. The agreement allows the facilitation of the origination of financing of JCB goods with NBC as the preferred financier and MTT as the supplier. Other are: NBC Head of Global Corporates, Wilson Nkuzi (behind Mr. Theobald) and MTT Limited General Manager, Yogesh Tripathi.
 The NBC Head of Corporate and Investment Banking, Theobald Sabi (left) exchange documents with Executive Director for MTT Limited which is the sole authorised dealer of JCB products in Tanzania, Mr Andrew Fimister (right) at an event where the two signed Preferred Supplier Agreement on behalf of their two organisations in Dar es Salaam on Friday. The agreement allows the facilitation of the origination of financing of JCB goods with NBC as the preferred financier and MTT as the supplier. Other are: NBC Head of Global Corporates, Wilson Nkuzi (second left) and MTT Limited General Manager, Yogesh Tripathi.


BASATA yatoa msukumo Tamasha la Krismasi

SERIKALI kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kuongeza ufanisi zaidi katika Tamasha la Krismasi mwaka huu kwa sababu  kupitia matamasha yake anafanikisha matakwa ya jamii yenye uhitaji maalum. 

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza alisema  kwa mwenendo huo bora unaofanywa na Msama anatoa wito kuendeleza mwenendo huo ili kuisaidia jamii.
 
Mungereza alisema Msama anafanikisha hayo kwa sababu anaipenda jamii ambako alitoa wito kwa wadau wa muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 hapa nchini ili kufikia malengo stahili.
 
Katibu huyo alisema mbali ya kuchangia jamii pia kupitia tamasha hilo wananchi  wa maeneo husika wanapata fursa nyingi katika maeneo yao kama madereva bodaboda, texi na biashara nyingine.
 
“Wananchi wa mikoa itakayofikiwa na tamasha hilo watambue kwamba ni lao, hivyo wajitokeze kwa wingi kwani viingilio vitakavyopatikana vinasaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, wajane, walemavu na wengineo,” alisema Mungereza.
 
Kuhusu waimbaji, Mungereza alisema waichukulie sanaa kwamba ni kazi  watumie vipaji vyao hasa wakifikiria jamii kwani wanahitajika kutoa elimu ya uraia kutoka kwao.
 
Katika hatua nyingine, Kampuni ya Msama imepokea kibali cha kufanikisha Tamasha la Krismasi mwaka huu ambako kampuni hiyo imejipanga kufanya tamasha hilo katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
 
Naye mmoja wa Watendaji wa Kampuni ya Msama, Jimmy Rwehumbiza aliyepokea kibali cha Tamasha la Kriamsi aliishukuru Basata kwa kufanikisha kibali sambamba na kupokea ushauri na mapendekezo yanayotolewa mara kwa mara yanayofanikisha matamasha hayo.


Haijapata kutokea vodacom nambari mbili mlipa kodi mkubwa nchini


Nusu ya fainali ya kwanza ya mashindano ya DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP katika uwanja wa Mwembe Yanga,Temeke

Nusu ya fainali ya kwanza ya mashindano ya DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP imepigwa hapo jana kwenye uwanja wa Bandari maeneo ya Tandika Mwembe Yanga kati ya Tabata FC na Black Six,mchezo ulimalizika kwa tabata kushinda bao 1-0 na kukata tiketi ya kucheza fainali hapo tarehe 29/11/2014 kwenye uwanja huo huo wa Bandari.mchezo huo uliweka rekodi ya mashindano ya NDONDO kwa kuhudhuliwa na mashabiki wengi.10553574_836086276455319_1176921432347220072_n Mashabiki wa BLACK SIX ya Buguruni.......... 1960140_836086329788647_6126915949753505475_nMshambuliaji wa YANGA Jerry Tegete alikuwa anaongoza mashambulizi ya timu yake ya nyumbani TABATA FC....... 10350425_836086403121973_4713464705511470346_nMkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Bwana Ruge Mutahaba,Fauzia Abdi pamoja Ibrahim Masoud 'Maestro' walikuwepo kushuhudia mpambano huo..... 
10382399_836086466455300_4570599094018049969_o
Nyomiiiii.....10408076_836086479788632_905767488845041078_nMpambano kati ya Tabata FC na Black Six ukiendelea kwenye uwanja wa BANDARI maeneo ya Tandika Mwembe YANGA ukiendelea...... 


KINANA: MUDA WA KULINDANA HAUPO TENA,AHITMISHA ZIARA YAKE MKOANI LINDI KWA KISHINDO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia CCM inasimamia uwajibikaji na kama mtu amekosea awajibike na akishindwa atawajibishwa mapema.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni chama pekee chenye mfumo ulioanzia chini hivyo watu waache unyonge Serikali hii ni ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa pongezi vijana Lindi waliojiunga na UVCCM mkoa wa Lindi kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini mkoa Lindi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi wa Lindi ni muda wa kuwaondoa wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Desemba mwaka huu kwa kuipigia kura CCM.
KWA BICHA ZAIDI BOFYA HAPA


TASWIRA KATIKA MAHAFALI YA TISA YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angellah Kairuki (kushoto), akimkabidhi cheti Muhitimu aliyefanya vizuri Shahada ya Kwanza ya Jinsia na Maendeleo, Nyamambara Simon katika Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika Dar es Salaam leo. W apili kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila.
 Wimbo wa Taifa ukiimbwa- Kutoka kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Maryam Abdallah Yusuph na Mjumbe wa Bodi Dk.Terezya Huvisa (MB).
 Vyeti vikiendelea kutolewa.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuku akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu na viongozi wa chuo hicho.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI


Mbunge wa Kigoma Kusini,mhe david kafulila na jessica kishoa wameremeta mjini uvinza

 Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila akiwa na mai waifu wake Jessica Kishoa wakijiandaa kukata utepe wa kuingia katika mnuso kwenye ukumbi wa Annex uliopo Uvinza, Kigoma,  jana Jumamosi Novemba 22, 2014
 Mhe David Kafulila akiwa kanisani  na mai waifu wake wa Jessica Kishoa wakati wa  kufunga ndoa katika kanisa la Roman Catholic katika Parokia ya uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014
 Mhe David Kafulila na mai waifu wake Jessica Kishoa pamoja na wapambe wao Mhe. Deo Filikujombe na mke wake Sarah Filikunjombe wakipeleka keki kwa wazazi wa bwana harusi 
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliopamba  harusi ya Mhe. David Kafulila katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Mhe Deo Filikunjombe. Mhe.David Kafulila ambaye ndiye Bw. Harusi, Mhe  Zitto Kabwe na Mhe David  Silinde. Picha zote na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma


Taswira mbali mbali za Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha (AGF)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa tatu kutoka kushoto) akizindua Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 20 Novemba 2014. Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sammy Mollel (kulia).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (kushoto) akihutubia wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake, washiriki (exhibitors) na wanunuzi wa madini ya vito ambao wamehudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yanayofanyika jijini humo kuanzia tarehe 18 hadi 20 Novemba, 2014.
Makamishna Wasaidizi wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini,wakifuatilia majadiliano uendelezaji endelevu wa madini ya Tanzanite nchini. Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini-Leseni, John Nayopa, Kamishna Msadizi wa Madini-Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane, na Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara, nchini Thailand, Tony Brooks akionesha machapisho mbalimbali kuhusu madini ya Vito kwa mgeni rasmi wa maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa pili kutoka kushoto), wengine ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa kwanza kutoka kushoto). Nchi ya Thailand ina uzoefu mkubwa katika uandaaji wa maonesho ya Vito ambapo wameshafanya maonesho zaidi ya 50 na wafanyabiashara wa madini ya Vito kutoka Tanzania wamekuwa wakishiriki Maonesho hayo.
Wachimbaji wadogo wa madini ya vito kutoka ukanda wa Umba mkoani Tanga waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha wakiwa kwenye banda wanalouzia madini hayo katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Pamoja nao ni Afisa Madini Mkazi mkoa wa Tanga, Mjiolojia Elias Kayandabila (wa nne kutoka kushoto).
Watendaji kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bruno Mteta, (wa pili kutoka kulia), Meneja Mipango na Utafiti, Julius Moshi (wa kwanza kulia), na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Eng. Yisambi Shiwa (wa tatu kutoka kushoto) waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito Arusha, wakisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Eng. Edwin Ngonyani (wa kwanza kushoto) aliyetembelea banda la Wakala huo katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Washiriki kutoka nchini Rwanda wakiwa na mgeni rasmi wa maonesho hayo ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa pili kutoka kulia), wengine ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa tatu kutoka kulia mstari wa mbele), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania, Richard Kasesera (wa nne kutoka kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sammy Mollel, (wa nne kutoka kulia_mstari wa mbele).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa kwanza kulia) akizungumza na mfanyabiashara wa madini nchini, Peter Pereirra mara alipotembelea banda la mfanyabiashara huyo katika Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha. Kulia kwa Naibu Katibu Mkuu ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja.