Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof Godius Khyarara ametoa rai kwa wale Wote walionunua nyumba za Mtoni Kijichi kukamilisha malipo ya nyumba hizo ndani ya siku 30 na kama hawatafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kunyang’anywa nyumba na kuuzwa kwa wanachama wengine.

Mkurugenzi Mkuu huyo alisema, wapo watu wameshikilia nyumba na hawajakamilisha malipo kama mkataba unavyosema na kusisitiza kuwa ndani ya mwezi mmoja kama mtu hajakamilisha malipo, masharti yote ya mkataba yatafuatwa.
Maagizo hayo aliyatoa wakati alipotembelea Miradi mbalimbali ya NSSF Ukiwemo mradi wa Dege Eco Village.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Prof. Godius Kahyarara (wa pili kulia), akiangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa nyumba za Dege Eco Village zilizopo Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Prof. Godius Kahyarara akifafanua jambo jijini Dar es Salaam, kuhusu wateja  walionunua nyumba za NSSF zilizopo Mtoni Kijichi kukamilisha malipo yao ndani ya siku 30 kabla ya hatua za kisheria hazijachuliwa kwa watakaoshindwa kufanya hivyo. Kushoto ni Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo.
 Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Godius Kahyarara.
 Baadhi ya wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village. 
 Meneja Kiongozi Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia) akifafanua jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara  alipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Prof. Godius Kahyarara (kulia) akiangalia moja ya nyumba zilizopo katika mradi wa Dege Eco Village.
 Sehemu ya jikoni.
 Sehemu ya jikoni.
 Ujenzi ukiwa unaendelea.
Nyumba za kisasa za Dege Eco Village.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...