TATIZO la usafiri katika jiji la Dar es Salaam linatarajia kupungua kufuatia kuanza kupindi cha mpito cha mabasi Yaendayo Haraka (BRT) mwezi ujao kufuatia kuwasili kwa mabasi 138 katika Bandari ya Dar es Salaam kutoa China tayari kwa huduma ya usafiri. 

 Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki aliwaambia waandishi wa habari jana wakati alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa mabasi hayo, kuwa wakazi wa Dar es Salaama kwa sasa wataanza kutumia usafiri wa mabasi hayo. 

 “Tumefikia hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri katika kipindi cha mpito," hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili", alisema na kuongezeas kuwa kampuni hiyo imepewa jukumu la kuendesha kipindi cha mpito ili waweze kupata uzoefu na zabuni ya mwendesha mradi kipindi cha kudumu itakapo tangazwa itasaidia wao kushindana. 

 Alisema serikali ilifanya kazi kubwa kuwainganisha Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya UDA-RT. 
 Aidha alikanusha kuwa nauli za mabasi hayo imepangwa kuwa Tsh. 900 zilizotolewa katika mitandao ya jamii, na kusema huo ni uzushi na upotoshaji na aliyefanya hivyo anatafutwa ili sheria ichukue mkondo. 
 Alisema suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) hivyo uzushi huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa kuwapuuzia. 

Msemaji wa Kampuni ya UDA Rapid Transit(UDA-RT),Bw,Subri Maburuki alisema mabasi yote yameingia yakiwemo ya mita 12 yapo 101 na mita 18 yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha mipito itanza baada ya kukamlisha taratibu za bandari. 

 “Tuliahidi kuwa mwezi huu wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni keli yamemekuja,” na kwa pamoja na yale ya kufundishi yatakuwa jumla mabasi 140", alisema Bw. Maburuki na kufafanua kwamba mabasi hayo yametokea kiwandani China na yanakidhi miundombinu ya barabara ya mradi wa BRT kama walivyokubaliana. 

 Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga alisema meli iliyobeba mabasi hayo ilipitia Kenya na kimsingi ilitokea China ilikuwa imebeba magari 1700 yakiwemo mabasi ya UDA-RT. 

 “Hatua hii ni ya msingi kwa nchi yetu, itasaidia wakazi kusafiri kwa urahisi na haraka,”alisema Bw. Mhanga. UDA-RT ni kampuni iliyoundwa na wazalendo kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri katika barabara ya DART jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki (kulia) akiwa katika bandari ya Dar es Salaam alipofanya ziara ya  kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) tayari kuanza kwa kuanza huduma ya kipindi cha mpito mwezi ujao. Kushoto ni Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni UDA Rapid Transit (UDA-RT),Bw. Robert Kisena ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wa pili kushoto ni Msemaji wa Kampuni hiyo,Bw, Sabri Maburuki.
 Sehemu ya  mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) yaliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya usafiri katika kipindi cha mpito kwenye miundombino ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka (BRT)kuanzaia mwezi ujao
 Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akijaribu basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam  kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika Kipindi cha mpito
Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akishuka katika basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam  kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mpito.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Sasa hayo makartasi ya plastiki humo kwenye viti si mngeyatowa tena kwa kujali risk ya suffocation just in case anything happen, au ndio hivyo tena walojisemea wahenga.... kipya kinyemi, japokuwa kidonda. By the way, natumai sasa suala la usafiri kwa wakazi wa Dar na maeneo ya jirani, utakuwa umerakhisishwa sana na kuwa wa haraka, wenye kueleweka na kutumainiwa ambao kwa kiasi kikubwa utawanufaisha sana wananchi katika harakati zao za kila siku za kwenda na kurudi hapa na pale kwa muda muafaka.

    ReplyDelete
  2. Bomba sana sasa haya ndiyo mabadiliko tunayo yataka ya vitendo

    ReplyDelete
  3. Kazi nzuri kabisa. Miaka ijayo msisahau reli ya jiji iboreshwe zaidi iwe ya kisasa na iwe na route za kila sehemu ya jiji ili wakazi wa jiji letu wanufaike. Addis Ababa wamezindua yao leo, reli ya umeme itakayowezesha watu milioni moja mjini humo kuitumia kila siku, hii iwepo kwenye mpango, wakati ukifika baadaye na uwezo ukiruhusu tuboreshe miundo mbinu hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...