Na Sylvester Raphael 
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla atembelea mkoa wa Kagera katika ziara ya kujione shughuli mbalimbali za Kanisa Katoliki mkoani zinavyotekelezwa pia na kutoa Baraka za pamoja kwa wakristo wa kanisa hilo. 
 Balozi Padilla akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Kagera alipowasili kumsalimia aliishukuru serikali ya mkoa wa Kagera kwa kuwaunganisha wananchi wa Kagera bila kujali imani zao ambapo wanafanya shughuli zao kila mmoja kwa imani yake bila usumbufu wowote. 
Pia Balozi Padilla alisema kuwa serikali inafanya kazi moja ya kuwaudumia wananchi pia na dini zinafanya kazi ya kuwahudumia wananchi hao hao kiroho kwa hiyo hakuna haja ya serikali na dini kugombana wala kukwaruzana kwasababu wote wanafanya kazi moja kwa wananchi. 
“Ni bora kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya serikali na dini na nashukuru jambo hilo linatekelezwa mkoani Kagera, nimekuja kukagua shughuli mbalimbali hapa na kupata baraka za pamoja na wakristo wa mkoa wa Kagera ili kujenga jamii moja yenye familia moja katika kumtukuza Mungu.” Alimalizia Balozi Padilla. 
Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella akimkaribisha Balozi Padilla alimshukuru kwa kufanya ziara mkoani Kagera na alimweleza kuwa serikali inatambua juhudi za kanisa Katoliki katika kuleta maendeleo kwa wananchi hasa ujenzi wa shule na hospitali kama huduma za jamii kwa wananch,i pia kutoa huduma za kiroho zinazosaidia kukuza maadili katika jamii. 
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa chini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla ziara yake imeanza leo Septemba 3, 2015 na anatarajia kuwepo mkoani hapa kwa takribani siku sita, aidha Balozi Padilla anatarajiwa kuongoza ibada takatifu ya maombezi ya Bikra Maria katika hija huko Nyakijooga Parokiani Mugana Wilayani Missenyi tarehe 6.09.2015 siku ya Jumapili.
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongela baada ya kumlaki alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Mkoa mjini Bukoba leo
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla, akitambulishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongela kwa viongozi mbalimbali wa mkoa alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera mjini Bukoba leo
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla, akisaini kitabu cha wageni  alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Mkoa mjini Bukoba leo
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongela akimkaribisha rasmi Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla, mjini Bukoba leo. Kulia ni badhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa na kushoto ni ujumbe wa viongozi wa dini alioongozana nao mgeni huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...