Mkurugenzi
Mtendaji Wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC),Juliet Kairuki
(kushoto) akizungumza machache katika mkutano baina ya TIC na uongozi wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ulioambatana na kutiliana saini
mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika kupeana taarifa na takwimu
ambao utakuza maslahi ya kiutendaji katika taasisi hizo.Wa pili kushoto
ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade.
Mkurugenzi
Mtendaji Wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC),Juliet Kairuki na
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade wakisaini
mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kupeana taarifa na
takwimu,ikiwa ni mpango utakaozipatia maslahi taasisi hizo.Mkataba huo ulisainiwa mwishoni mwa wiki
kwenye Ofisi za TIC,jijini Dar es Salaam.Wengine pichani toka kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Nakuala
Senzia,Mwanasheria wa TIC,Alex Mnyami,Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa
TIC,Pascal Maganga,Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti wa TIC,Anna Lyimo pamoja
na Mkurugenzi wa Elimu kwa Walipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA),Richard Kayombo.
Mkurugenzi
Mtendaji Wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC),Juliet Kairuki na
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade
wakibadilishana mikataba hiyo mara baada ya kuisaini, kwenye Ofisi za TIC,jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa
wa Kituo cha TRA ndani ya TIC,Adam Lingwetu (kulia) akifafanya jambo
juu ya machine maalum ya kutoa Namba za TIN wakati wa mkutano baina ya
TIC na uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za TIC,jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...