Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu maalumu ya kutembelea maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino nchini ambapo timu hiyo inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa kuanza na mikoa sugu ya matukio hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora na Shinyanga na baadaye itafuata mikoa mingine. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Picha na Emmanuel Massaka

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

Serikali imewapiga marufuku waganga wa jadi wanaotumia ramli kutokana na kuwa chanzo cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Mambo Ndani ,Mathias Chikawe wakati alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam,Chikawe amesema waganga wa jadi wanaotumia ramli wamekuwa wakiwaambia watu kuwa kuua au kupata kiungo cha albino ni utajiri,kuwa mvuvi wa mwenye mafanikio.

Chikawe amesema Jeshi la Polisi na Chama Cha Wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) wameunda timu maalum ya kufanya operesheni kwa waganga hao katika mikoa mitatu ikiwa lengo ni kutokomeza mauji ya albino.

“Tunataka kutokomeza mauaji ya Albino kwa timu hii ambayo tumeiunda itapita kila sehemu na wale wote ambao watabainika watachukuliwa hatua na kesi hizo zitapewa kipaumbele na Mwendesha Mashitaka Nchini (DPP)”alisema Chikawe.

Operesheni hiyo ya kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) itafanyika katika Mikoa mitano ambayo inaonekana ni sugu katika matukio hayo, nayo ni Mwanza,Tabora,Simiyu,Shinyanga pamoja na Geita.

Aidha alisema kuhusu serikali kutoamini ushirikina wa kazi hiyo pia itafanywa pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Mikoa na Tawala za Mitaa (Tamisemi) ambapo sheria ya  kuwabana itakapopatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hata viongozi wa dini wanaohamasisha fujo na vurugu wafungiwe. hawana tofauti na waganga wa kinyeji kwani yote ime-base kwenye imani. au kwa vile hao wana pesa wanajua namna ya kupitisha mambo yao

    ReplyDelete
  2. Dah...twafa sasa tutakula wapi jamani tena mbaya zaidi mmesubiri 2015 ndio mnaanza fitna zenu....mngesubiri basi walau baada ya Oktoba ndio mpitishe amri hiii........

    ReplyDelete
  3. Nchi hii bwana sasa mtajuaje kama sheria au amri inafuatwa??mtawafuata mpaka vibandani? au mtawawekea ntelijensia??haya yetu macho.....

    ReplyDelete
  4. Dah! ingawa nakataza ramli sasa sijui nitapita Ubunge?? Alafu sijui kama nitakuwepo kwenye baraza la Rais mpya? Au nigaili nini kutoa hii kauli anyway poa tu ngoja wabongo watulie alafu tutatoa vibali kwa wapiga ramli wote. fanya mchezo kwenda mlingotini?? si tutakufa gafla!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...