Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’  kupitia kwa mawakala  wa ‘FahariHuduma’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.

Alisema kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.

“Tunataka kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,”.

Akielezea namna ya kushiriki  na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dk. Kimei alisema kuwa shindano hilo ni la wateja wote wa CRDB watumiao huduma hizo na mshindi atakuwa ni yule mwenye miamala mingi zaidi kwa mwezi husika.

“Mshindi ni yule atakayekuwa amefanya miamala mingi zaidi kwa kutumia SimBanking au FahariHuduma katika mwezi husika, iwe ni kutumia fedha kwenda kwenye akaunti nyingine, au kwenda kwenye mitandao ya simu au kulipia Ankara,” alisema.

Kwa upande wake ,Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari alisema ubunifu ndio njia pekee itakayotatua changamoto, ni muda muafaka kwa Watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kujishindia zawadi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo mtumaji wa miamala mingi katika benki hiyo atapata zawadi ya gari aina ya Passo. Kulia ni mjumbe wa bodi, Celina Mkoni.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na SimBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...