Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omar Mjenga leo ametembelea kampuni ya Nyumba ya NAKHEEL, ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai, kwa lengo la kujionea miradi mikubwa iliyotekelezwa na kampuni hiyo.

Baadhi ya miradi iliyosimamiwa na kampuni hiyo ni pamoja na The Palm Dubai (the largest island Palm City in the World), Nakheel Mall, Dragon Mart na baadhi ya hotel za nyota tano Jijini Dubai.

Kufuatia mazungumzo kati ya Mhe. Mjenga na Bw. Rashid Lootah, mwenyekiti wa NAKHEEL, wamekubaliana kwa pamoja kuwa mwenyekiti huyo na ujumbe wa washauri na wataalam wake kufanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania, tarehe 10 hadi 13 Agosti, 2014.

Wakiongozana na Mhe. Balozi Mdogo Mjenga, watakutana na taasisi mbali mbali zikiwamo NHC, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), TTB, TANAPA na zingine nyingi. Aidha, watapata fursa ya kuongea na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Viwanda na Biashara, Ardhi, 
Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

Kampuni hii ina nia ya kuwekeza katika hotel za nyota tano, nyumba za makazi na biashara pamoja na maduka makubwa(shopping malls).
 Mifano ya majengo ya kampuni hiyo
 Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, alipotembelea kampuni ya Nyumba ya NAKHEEL
 The Palm Dubai (the largest island Palm City in the World

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2014

    Uje uwekeze na mutufindishe ili tujitegemee na siye tujenge nyumba bora

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...