WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameawaonya baadhi ya Watanzania wanaokuja katika jiji la Guangzhou nchini China kwa ajili ya kununua bidhaa mbalimbali waache kuuza hati zao za kusafiria kwa raia wa nchi nyingine kama njia ya kujiongeza kipato. 
 Ametoa onyo hilo jana usiku (Alhamisi, Oktoba 24, 2013) wakati akizungumza Watanzania wanaofanya biashara na wale wanaoishi katika jiji la Guangzhou, jimbo la Guangdong ambalo ni jiji kubwa la biashara lililoko kusini mwa China. 
 Alisema kuwa wengi wa wafanyabiashara hao wanapouza pasipoti zao wanasingizia kuwa zimepotea ndio maana kuna malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania wanaofika katika jimbo hilo kudai wanaibiwa hati zao za kusafiria wakati sio kweli. 
 Wakati wa mazungumzo hayo, mmoja wa Watanzania hao aliyejitambulisha kwa jina la Ambrose Lugai alisema changamoto nyingi zinazowakabili Watanzania waishio katika jimbo hilo na moja ya tatizo hilo ni kuibiwa kwa hati za kusafiria za Watanzania. Bw. Lugai alisema tatizo la wafanyabiashara wengi kupoteza pasipoti limekuwa sugu na kila siku linaongezeka na cha ajabu linawatokea wafanyabiashara wa kutoka Tanzania tu. 
 “Hatuwezi kusema ni u-carelessnes, lakini jamii ya hapa ni kutoka mataifa mbalimbali, inakuwaje pasipoti za Tanzania tu ndio zinakuwa hot cake, naomba utusaidie namna ya kulinda hati hizi,” alisema Bw. Lugai. 
 Alimwomba Waziri Mkuu awasaidie kuzungumza na Serikali ya jimbo hilo ili Watanzania wawe wanaacha pasipoti hotelini wakati wanapoenda mitaani, badala yake wapewe karatasi nyingine ya kuwatambulisha huko mitaani. Katika kujibu hoja hiyo ya Bw. Lugai, Waziri Mkuu alisema kwamba suala hilo linamshangaza kwamba inakuwaje hati za wafanyabiashara wa Tanzania tu ndio zinaiibiwa wakati wafanyabiashara wanaofika kwenye jimbo hilo ni wengi kutoka mataifa mbalimbali. 
“Kupoteza pasipoti ni jambo la nadra sana, sio la kawaida. Nilitegemea hili linaweza kumtokea mtu mmoja mmoja, lakini nashangazwa kwamba hapa Goangzhou ni tatizo kubwa.” “Lakini taarifa nilizo nazo nyie wenyewe wafanyabiashara mnauza hati zenu kwa Wanaigeria ili mpate fedha za kufanyia biashara. Ndio maana nawasihi achani haya mambo, mnajifedhehesha wenyewe na mnaifedhehesha nchi,” alisema Waziri Mkuu. 
 Alisema kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa na akamtaka balozi wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali mstaafu Abdulrahman Shimbo afuatilie kwa karibu kujua idadi ya watu walioibiwa hati zao za kusafiria ili Serikali iweze kulishughulikia. 
“Lakini nawaonya acheni tabia mbaya ya kuuza pasipoti zenu kwa tamaa ya kupata vijipesa vidogo vidogo hivyo, hii ni kuivunjia nchi heshima,” alisema. 
 Lakini pia alitaka jumuiya ya Watanzania waishio China kuimarishwa zaidi ili wawe na uwezo wa kushughulikia kero zao mbalimbali zinazowakabili wakiwa katika ugenini. 
Alisema ni kuimarika kwa jumuiya hiyo tu kutawasaidia wanafunzi na wafanyabiashara kufikisha malalamiko yao haraka serikalini. 
 IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
IJUMAA, OKTOBA 25, 2013
Waziri Mkuu, mizengo Pinda akiongozana na Mwenyekiti wa shirika la Ndege la China la HAINAN AIRLINES, Bw. Chen Feng (kushoto na Balozi wa China nchini Dr. Lu baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Dong Fang mjini Guanzhou akiwa katika ziara ya kikazi nchinio China Oktoba 24, 2013.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harison Mwakyembe akibadilishana kadi za mawasiliano na Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la China Southern Air, Bw. Tan Wengeng wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake walipokutana na Rais uyo kwenye Hoteli ya Dong Fang mjni Guanzhou China Oktoba 24, 2013.
Waziri Mkuu, MIzengo Pinda akisalimiana na Gavana wa jimbo la Guangdong nchini China, Bw. Zhu Xiaodan kabla ya mazungungumzo yao kwenye hoteli ya Dong Fang mjini Guanzhou akiwa katika ziara ya kikazi nchini China Oktoba 24, 2013.
Watanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao mjini Guanzhou China akiwa katika ziara ya kikazi Oktoba 24,2013.
Rais wa Umoja wa Watanznia waishio Guanzhou China, John Rwehumbiza akitembea haraka kuwahi mkutano kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na watanzania waisio Guanzhou Oktoba 24, 2013.
Watanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao mjini Guanzhou China akiwa katika ziara ya kikazi Oktoba 24,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Watanzania waishio Guanzhou China baada ya kuzungumza nao akiwa katika ziara ya kikazi nchini China Oktoba 24, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Haya sasa watanzania wafanya biashara na wakazi hapo Guanzhou,hii kauli ya Waziri Mkuu ina ukweli?

    Nilitegemea mtoe maoni hapa ili hii sintofaham itoweke.

    Baadhi kwa tamaa zenu mnatuharibia jina jema la Tanzania mbele ya mataifa mengine.

    Ama ndio yale yale "Lisemwalo lipo na kama......

    ReplyDelete
  2. Jamani tanzania ya leo inahitaji watu wanaofikiria zaidi ili kuikomboa la sivyo usanii unaoshabikiwa na kulindwa na viongozi wetu na short cut inayoonekana kushamili ya kutafuta mali kwa kuuza madawa na hayo ya kuuza passport na mengine ni maadili ya nchi yaliyoporomoka na yanahitaji solution from grass root la sivyo tukiyalea utakuwa ndo utamaduni wa taifa letu. Tunajenga jina baya kwa kukosa maadili na taratibu tunaanza kuiandika record kama Nigeria. ila inasikitisha viongozi hawalioni na kama wanaliona hawana majibu.Mimi nadhani tunahitaji research zaidi ifanyike ila kwa mtazamo wangu hiki kizazi ndo kwisha tunahitaji tuanze kujenga maadili kwa watoto wetu na hasa kwa kuwafundisha kuheshimu principle za maisha you may wonder by not knowing how it will impact on next generation.hatujali elimu tunayowapa watoto na makuzi ya wanetu ni muhimu kujenga taifa zuri lenye maadili.

    ReplyDelete
  3. Bibo anza dieting na tizi, kweli basketball utaweza kweli wewe.

    ReplyDelete
  4. Hapo Mkuu kasema ukweli.Iweje waTZ wapoteze pp ? Tatizo la kutaka dezo...hadi kutuletea bidhaa feki.

    ReplyDelete
  5. Basi, tupigiane simu hata usiku wa manane!

    ReplyDelete
  6. Mbongo kauza Passport kwa dola$2000 ,Mnaigeria (MPOPO) kaitumia Passport ya kibongo kubebea unga.
    Mbongo anapewa passport mpya maisha yanaendelea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...