Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi jijini jana


Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, amekiri kuanzisha Kampuni yaumeme wa upepo ya Power Pool East Afrika Ltd, kutokana na anachokiitagharama zitokanazo na mitambo ya kukodi.
Amesema mkataba wa serikali na Kampuni ya Independent Power TanzaniaLimited (IPTL) wa miaka 20 ni mzigo mzito kwa serikali na taifa kwaujumla, kwa kuwa unataka Tanesco ndiyo inunue mafuta ya dizeli, vipurina gharama za mashine.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakyembealisema pamoja na hilo, bado Serikali ya Tanzania inatakiwa pia kuilipa IPTL Sh bilioni 3.7 kwa mwezi ambayo ni sawa na Sh milioni103.7 kwa siku.
“Jamani huu ni mzigo mzito kwa Watanzania tena kuubeba kwa miaka 20,ndipo kwa uchungu tuliona na tukaamua tufikirie njia mbadala yakuwaondolea Watanzania mzigo huu,” alisema.
Alisema waliamua kuanzisha kampuni hiyo, mwaka 2004 baada ya kuchapishwa kitabu cha UglyMalaysian ambacho kilikuwa kinausema vibaya mkataba wa Tanesco na IPTL hasa suala la gharama za uendeshaji mitambo.
Miongoni mwa washirika wengine wa Mwakyembe katika kampuni hiyo ni Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa, ambaye ni Mjumbe wa Bodi yaWakurugenzi wa Tanesco.
Wengine ni Emmanuel Kasyanju, Prosper Tesha,TBC (1998) Limited, Isaac Mwamango, Mwacha Kagoswe, Josephine Pinana Athumani Ngwilizi, MECCO Limited ya Maungo Kwabibi, BestonMwakalinga, Niels Dahlmann na Leonard Tenende.
Dk. Mwakyembe alisema IPTL ilinunua mitambo yake kwa dola milioni 120za Marekani lakini kutokana na fedha nyingi ilizokuwa ikilipwa kwasiku, baada ya miezi minne inaweza kununua mitambo mingine kama hiyo.“Huu ni unyonyaji hatuwezi kuuvumilia.”
Alisema kwa upande wa Dowans,hali ni tofauti kwa kuwa hakuna hata mkataba, mitambo yake ni mibovu tofauti na ya IPTL, imeishitaki Tanesco, inadaiwa na benki nyingi naTanesco wenyewe wanadaiwa.
“Sasa jamani utanunua kitu chenye matatizo?”
Alisema kampuni nyingineza umeme zimekuwa zikiila nchi kupitia mtindo huo akitolea mfano waAggreko ambayo inalipwa Sh milioni 62, APR Mwanza Sh milioni 76, Dowans Sh milioni 158 na Songas ambayo bado inalipwa Sh milioni 265 zote ni kwa siku.
Alisema akiwa na wenzake wengi wakiwamo maprofesa, wahandisi naviongozi wengine wa siasa, waliamua kutafuta suluhu la tatizo hilo kwa kuanza mchakato wa kuanzisha kampuni ya umeme wa upepo ambayo inatarajiwa kuzalisha megawati 1,800.
Alisema kwa kuwa bado kampuni hiyo iko kwenye mchakato na haijaanza kuzalisha, hawezi kuelezea maslahi yake juu ya kampuni hiyo na kwamba kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule kuchunguza Richmond na kuzungumzia suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans, havina uhusiano wakimaslahi na kampuni hiyo ya umeme wa upepo.
Alisema kwa sasa wanahitaji mitambo na Sh nusu trilioni, ili wawezekuanza kuzalisha umeme.
“Kampuni hii ni ya watu masikini hawana fedhani ndoto kuzipata hizo nusu trilioni lakini tunajitahidi, hivyo siweziku-declare interest (kueleza uhusiano wangu) ni sawa na mkeo akiwa namimba uanze kutangaza kuwa mtoto wako atakuwa daktari.
”Aliwataka Watanzania kuelewa kuwa maslahi ya nchi yao yatazingatiwa naWatanzania wenyewe na ndiyo maana wao wako katika mapambano, kwanikilichotokea ni moja ya mapambano na hawataacha kupambana.
Akijibuswali juu ya yeye akiwa kiongozi kujihusisha na biashara, alisemaiwapo mradi huo utaanza kuzalisha umeme, atachagua aende wapi, kwenyeubunge au kuwa mfanyabiashara.
“Lakini naamini kuwa ubunge si kazi ya kudumu japo kwa upande wangusina ukomo na kazi hii, ila ifahamike kuwa sina mkataba na Bunge.
”Kuhusu madai yaliyoandikwa na chombo kimoja cha habari kuwa ameumbuka,alisema hawezi, hana sababu na wala hatarajii kuumbuka, hasa kutokanana ukweli kuwa tuhuma hizo zimetolewa na chombo cha habari cha Mbungewa Igunga, Rostam Aziz.
Hata hivyo, Rostam naye alidai kuwa yeye si mwandishi wa habari hivyo kama Mwakyembe anatuhumiwa kwenye vyombo vyake vya habari, anatakiwa ajibu hoja na si kumtafuta au kumwandama mtu.
Akizungumza na waandishiwa habari leo Dar es Salaam, Mwakyembe alisema imezuka tabia ya baadhiya viongozi waliochafuliwa katika jamii, kutumia vyombo kujisafisha, lakini kwa mtindo wa kuwachafua wengine.
Alisema kwa wanaomtuhumu kwa kutetea ununuzi wa mitambo ya IPTL nakumshangaa anapogomea ununuzi wa mitambo ya Dowans, wafahamu kuwakampuni hizo mbili hazifanani wala mazingira yake hayahusiani. “Nikama usiku na mchana.”
Dk. Mwakyembe alisema IPTL ilikuwa na mkatabana Tanesco tangu Mei 26, 1995, lakini kutokana na mvutano, umemeulianza kuzalishwa Januari 2002 na mkataba huo ni moja ya mikatabaambayo Kamati Teule ilipendekeza serikali iipitie upya.
Akijibu swali juu ya namna atakavyoshirikiana na Rostam wakiwa wanaCCM katika uchaguzi hata baada ya kuchafuana, alisema yeye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu sawa na Rostam.
“Muulizeni mwenyewe kwa nini anatuma vijana wake kuchafua wenzake analifikiriaje hilo!”
Aliviasa vyombo vya habari kutumia fursa walizonazo kuokoa taaluma hiyo ambayokwa mujibu wake, inaelekea pabaya, akitolea mfano alivyotumiwa kwenyebarua pepe, habari ya kummaliza, hali iliyomfanya atambue kuwa taalumahiyo imeingiliwa.
Alisema suala hilo lote ni jambo dogo, lakini limekuzwa kutokana namaslahi ya watu ambayo yangepaswa kujadiliwa bungeni.
“Tumelikuzakupita kiasi, issue (masuala) za Bunge zimalizikie bungeni na sikwenye magazeti yetu … ya bungeni yaishie bungeni.”
Kwa upande wake,Rostam alisema kwanza yeye si gazeti wala mwandishi wa habari na walahaelewi chochote ila kama Mwakyembe amekiri kumiliki kampuni ni kwelimgongano wa maslahi kwa vyovyote vile utakuwapo.
“Sitaki kuzungumza zaidi ila nasema mimi si mwandishi na kama Dk.Mwakyembe ameandikwa kwenye gazeti, basi ajibu hoja asianze kutafutawatu au kuwaandama,” alisema Rostam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Hongera dk. Mwekyembe wazo ni zuri naomba mungu awape nguvu muondoe wazo kwenye makaratasi liende kwenye uhalisia,megawati 1800 kwa umeme wa upepo mtaleta unafuu kweli.Taaluma ya uandishi wa habari Michuzi imeingiliwa na mafisadi baadhi wanatumiwa vibaya kubalini,dowans wapeleke mitambo yao kwenye CHUMA CHAKAVU!kila la kheri

    ReplyDelete
  2. mwanasheria wa serikali anafanya kazi gani? Hiyo mikataba si kui-frustrate tu jamani. Pesa mingi ivyo. Yani lazima kuna ulaji unaondelea hapo na MIKONO ya watu kibao inashikilia hii mikataba. Tunahitaji muangaza zaidi ndani ya serikali...tungefurahi kujua zaidi juu ya hii topic bwana Michu

    mtoto

    ReplyDelete
  3. Huyu ndugu amefanya kazi kubwa sana katika historia ya ufisadi tanzania na mimi ni mshabiki wake mkubwa sana.Lakini hapa kuna tatizo,majibu yakuridhisha yanahitajika hata kama wanaomkomalia ni maadui zake kisiasa.Kuna mgongano wa kimaslahi wa dhahiri.

    ReplyDelete
  4. Hata kama anauchungu huo kwa nchi, ila hapo alikosea kutoweka bayana kuhusu kampuni yake, kwani kuna ''conflict of interest'' Especially alivyoongelea Richmond kwa uchungu kama vile! Je, hawakuwa na ugomvikweli kwakuwa kampuni yake ilianzishwa mapema kuliko hiyo Richmond feki ambayo ilipata tender na yeye kukosa!? Maana hawa watu ndio wameanza kumchokonoa na hatujui wana lipi zaidi baada ya yeye kujibu! Je, wakija na ushahidi kuwa aliomba tender na akakosa!?.............definatetly itakuwa ''conflict of interest and lack of trust!'' Kwa position aliyokuwa nayo alitakiwa atafute njia yeyote ile ya kufahamisha umma kuwa ana kampuni kama hiyo (tena yeye ni mmoja wa hisa kubwa). Hilo ni wazo tu!

    ReplyDelete
  5. It doesnt matter hata kama kuna mgongano wa kimaslahi, alimradi kama huo mradi utaleta hauweni kwa watanzania basi tupo nyuma yake. Tunachotaka watanzania sio siasa ila auweni, manake umeme umekuwa ni tatizo. Mwakyembe tupo nyuma yako.

    ReplyDelete
  6. Nae anaharufu ya ufisadi.
    1. Ana conflict of interest wakati akishika kuchunguza mikataba ya umeme.

    2. Hata interest iweje, position aliokuwa nayo kama mweneykiti wa kamati ya kuchunguza Richmond na hata ile ya unaibu wenyekiti wa kamati ya nishati imempa acess ya information kwa manufaa ya kampuni yake.

    3.Kupendekeza kuvunjwa kwa taratibu za ununuzi ili inunuliwe IPTL ni kuhujumu sheria ambayo bunge imezipitisha. Alipendekeza kununua mitumba ya IPTL

    4. Sababu za kupendekeza kununua mitambo ya IPTL ni hizo hizo za kukubali au kukataa kununua mitambo ya Dowans.

    5.Sababu hizi zimemvua heshima na kumuacha bila ya nguo katika taaluma yake ya sheria.

    6. Kumbe ukali wote dhidi ya Rashidi ni vikumbo kati yake na Rostam --- wote mawakala wa ufisadi. Labda mmoja ni mkubwa wa siku nyingi na mwingine ni dogo, lakini yumo.

    ReplyDelete
  7. Hivi nchi yetu ta Tanzania hakuna regulation zozote za kuhakikisha watu hawaharibiani majina na kuandika chochote wanachokitaka.Mwakyembe ni mchapa kazi lakini hapo kuna "conflict of interest" kama anataka kufanya biashara ni sawa afanye lakini asitumie jukwaa la siasa kuhakikisha anapata anachotaka ndio achague kufanya Biashara au siasa kama kufanya uamuzi afanye sasa.

    kwanini tunaona wanasiasa wengi wanaingia Bungeni kwa maslai ya kufanya Biashara na sio kuwatumikia wananchi waliowachagua.Kwani bila ya yeye kujiunga kwenye siasa asingewapata hao marafiki wanaotaka kuanzisha huo mradi japo mradi ni wazo zuri sana.

    Kenge

    ReplyDelete
  8. Wanaodhani kwamba Mwakyembe ana conflict of interest nawashangaa sana. Mimi siioni kabisa, instead nimegundua kumbe ni mwanasiasa ambaye 'anapractice what he preaches'. to fauti na wengine.
    inatakiwa kila sera iwe implemented na sera ya kutunza mazingira itatekelezwa na nani kama si watanzania wanaojitolea kwa mali zao kutekeleza? hao wote wanaoupigania umeme wa gesi, wa generators za mafuta, wako short sighted, umeme wa upepo ndio mkombozi wetu pamoja na sola. mungu awabariki, tuko nyuma yenu.
    hii ni vita ngumu Dr.M.
    Kupigana na matajiri selfish ambao hawajali wataachia nini watoto wao ni kama vita dhidi ya sigara, visingizio vingi sana, eti mara kodi, mara ajira, mara eti wana chuki binafsi, ila tutafika tu.
    GOODNESS WILL PREVAIL

    ReplyDelete
  9. Utumwa, utumwa, utumwa!!! umerudi Rostam alikuja kutafuta watumwa miaka ile ya giza akawapata akawauza kadri alivyoweza na akatajirika. Nuru ikaingia, biashara ya utumwa ikakoma. Sasa giza limerudi na biashara ya utumwa imerudi kwa Ali mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya na wengi, wakiwemo waandishi wa habari wameshanaswa kwenye huu munyororo wa utumwa. Nadhani ipo haja ya kuikomboa nchi kwa mara ya pili kwani utumwa huu ni mbaya sana kuliko ule wa awali.

    ReplyDelete
  10. Wanasiasa miaka hii is for personal interest to make big money na sio kulitumikia Taifa. Watu aina ya akina Nyerere ni wachache. Utakuta kila mtu ana biashara ya mabilioni kwanini basi unafuu au faida yoyote isiwe ni kwa manufaa ya wananchi? JK aliposema kwamba chagua biashara au uongozi alikuwa sawa kwani huwa haviendi pamoja. Nia hapa ni kujinufaisha na sio kutafutia wananchi unafuu na kama ni hivyo basi tumia njia zinazoeleweka na sio kampuni binafsi

    ReplyDelete
  11. Huyu Dr.kachafuka tu.hadhi yake inaendelea kushuka hata ajishebedue vipi.Njaa mbaya jamani.Baada ya kuingia ktk kamati ndo aliziona write-up kibao za Tanesco na wizarani ndo naye alicapitalize!.
    namshauri ukitupia wenzako mawe ukiwa ktk nyumba ya vioo ndo hayo.
    Watanzania wa leo sio mabwege tena.Usemi wako umekushushua mwenyewe.Ushauri nasaha ajiunge na mipasho! ameonyesha anaweza vidole juu! Mwombe radhi Zitto, sababu za IPTL hazitoshi.Tupe nondo kama za kamati teule na sio blah blah

    ReplyDelete
  12. Sitaki kuamini kuwa pamoja na mwakembye kutoa maelezo yale jana kuna watu hawajaelewa. Hivi conflict of interest inakujaje kwenye kampuni na project. wao wameandaa project wakaipromote wakatokea watu wakatake over hivi ni kitu gani kigumu kuelewa hapo jamani ndio maana akawaambia waandishi wawe wanafanya home kwanza kabla ya kukurupuka.

    ReplyDelete
  13. mwe kyala akutule Mwakyembe!

    hivi ukamewke rositamu azizi na mwekyembe wa kyela mwi Itete wana fanana kweli jamani hata kidogo! one is pure Tanganyika guy and the other mmmmmh sory I cant even say it! we vote for mwakyembe jamani laki annoy wa soa nda so kasema upope na gas mazingira vip? labda ni challange tu kwa rostamu lakini tukijiwezesha tutaweza TANGANYIKA HOYEEEEEEEEEEEEEEEE
    nyie wabeba mabox hamjui adha ya umeme sasa mi ni kmazi wa kinzudi kweli nguzo moja ni 1.4250M KWA MI MTAZANIA HALISI SI BORA UMEME WA UPEPO KWELI JAMANI ? SITAKI MMMMM ? KAMA HUAMINI BASI MWAMBIE MICHUZI AENDE KINZUDI ATAKUTANA NA VIBATARI WE ACHA TUUUUU

    ReplyDelete
  14. Inashangaza Kinzudi inapokosa umeme wakati kuna mitambo jirani tu pale Salasala. Suala la conflict of interest katika hili liko kwenye "gray area". Kwa upande mmoja kitendo cha kuwepo wazalisha umeme wengine kinaweza kuathiri uwezo wa mitambo ya Mwakyembe and company kuuza umeme wake kwa Tanesco. Kwa upande mwingine bado kuna pengo kubwa kati ya kiasi cha umeme kinachopatikana na kinachohitajika kiasi kwamba bado kuna nafasi za kuiuzia Tanesco umeme kwa faida. Ingekuwa hii habari imetolewa kwa mara ya kwanza na chombo cha habari ambacho nina imani nacho yaani magazeti tofauti na magazeti ya Rostam ningeona kuna conflict of interest. Lakini kwa kuwa habari imeanzia kwenye magazeti ya Rostam naona kama hizi ni hasira za Richmond tu.

    ReplyDelete
  15. KWELI HAKUNA CHENYE MWANZO AMBACHO HAKINA MWISHO.ATIMAYE SASA WANA SHAMBULIANA WENYEWE KWA WENYEWE SASA NA KUTISHIANA KUTOLEANA SIRI ZAO.KWELI SAFARI YETU YA KUJIGOMBOA KUTOKA KWA VIONGOZI WABOVU INAFIKIA MWISHO KARIBUNI.
    Mdau "cha mtu mavi"

    ReplyDelete
  16. Huu ndio wakati wa Tanzania na watanzania kuporomoka hasa.
    Kila mwanasiasa kazi ni hii tu ya kuita mikutano na waandishi.
    Na kinachozungumzwa ni kashfa baina ya wanasiasa na wabunge wa chama kile kile.
    Tutafika wapi?
    Kuna wakati nilishawishika kuamini kuwa Mwakyembe ni mmoja wa wakombozi wapya wa Tanzania na watu wake.
    Sasa nimevunjika moyo, sana sana tu kanikumbusha siku William Gallas wa Arsenal alipolikoroga kwa kushambulia wachezaji wake wakamnyang'anya ukapteni.
    Siwezi kuamini kuwa wanasiasa wa TZ ni washamba kiasi hiki.
    MWAKYEMBE JIUZULU, unanyea kambi, ni petroli ndani ya chama chako, unavunja mshikamano, siasa huiwezi.
    Mndengereko wa Ukerewe

    ReplyDelete
  17. Jamani tumekwisha, hata yeye ni fisadi pamoja na mbwembe zote zile bungeni.

    Amekiri kuwa na (minority) interest wakati akichunguza mkataba waa Richmond.

    Kama mweneykiti wa kamati ya kuchunguza Richmond na hata ile ya unaibu wenyekiti wa kamati ya nishati imempa nafasi ya kupata taarfia kadhaa kwa manufaa ya kampuni yake.

    Pamoja na Shelukindo alipendekeza kuvunja sheria (PPA)kununua mitambo chakavu ya IPTL

    Alipendekeza kuwa kwa vile mitambo ya IPTL haifai ifanyiwe urekebishaji itumie gesi ya songongo - kama vile yeye ni engineer. Kisa? - ufisimaji!!

    Kumbe sheria inayokataza kununua mitambo ya IPTL ndio hiyo hiyo inakataza kununua mitamba ya Dowans.

    Kama professor wa sheria, hesima ya conflict of interest na ile ya kushauri bunge na serikali kuvunjwa sheria ni kosa kubwa!!!

    Sina hamu na viongozi wetu.

    ReplyDelete
  18. Nchi imekwisha!!

    Kumbe hata huyu ndivyo alivyo!!!

    Yaani alikuwa mstari wa mbele kukaba Richmond na Dowans wakati yeye mwenyewe ana interest zake katika hiyo sekta.

    Nchi zenye maadili huwzi kupata nafasi ya kuumiza wapinzani wako wa kibiashara kwa kutumia mgongo wa Ubunge.

    Kuna actual and perceived conflict of interests, zote ni ufisadi.

    Kumbe anataka yeye ale!!!

    ReplyDelete
  19. Salam mbunge wa nanihi.Nimwezi mmoja sasa nimekua nikifuatila malumbano ya tatizo la tazizo la ununuzi wa mitambo ya kufua umeme,kununua au kutonunua mitambo ya dawons hivi sasa kiasi cha megawatts 140 zimeishatoka katika grid ya taifa kutokana na kuvujwa kwa mikataba au kuisha kwa mikataba ya makampuni yaliyokua yakifua umeme tuachoshuhudia ni malumbano sijasikia kauli ya serikali ni mikakati ipi au mipango inayoendelea kiziba pengo hili au kutatua tatizo hili.au tunasubiri giza ndipo hatua za dharula zitakapochukuliwa kuitafuta Richmond nyingine?Kwani katika dharula ni ni lahisi kwa mafisadi kupenyeza mipango yao ya kujineemesha.Rais,Waziri mkuu ,bunge mko wapi inasikitisha au inahitaji maandamano ya walalahoi ili baadae iundwe tume n.k.Sasa sio wakati wa malumbano ni wakati wa kuchukua hatua.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  20. MUNGU INUSURU TZ.YETU HAAA?HILI MWAKYEMBYE MWEMBWE ZOTE ZILE KUMBE NALO FISADI,
    KWELI KIKWETE JINIAZI KUWATOA NJE WANASIASA NA KUFANYA BIASHARA ALILIJUA HILI KUA UNAFKI UTAKUEPO KTK KUJAJI MASLAHI YA KWELI YA TAIFA
    NYINYI MNAO MTETE MWAKYEMBE KWA UKABILA WENU ACHENI UPUUZI WENU MAANA HAKUNA MTAKACHO FAIDIKA ZAIDI YA BIBI ZENU NA WAJOMBA ZENU NA TAIFA KWA UJUMLA KUWA MASKINI
    UZALENDO HAUTIZAMWI KWA RANGI BALI UZALENDO WA KUTOKUA MNAFKI UIPENDE NCHI KWA DHATI
    MAANA TUKITAKA KUTIZAMA RANGI HUYO MWAKYEMBE ANAWEZA KUA NI MZAMBIA AMA MMALAWI
    ONDOENI UPUZI WENU HAPA KUTETEA WANAFKI WANAOWEKA MASLAHI YAO BINAFSI BADALA YA TAIFA NA KUWADANGANYA WASIO NA ELIMU KAMA NYINYI
    LAKINI HATUWEZI KUSHANGAA KUTOKANA NA ASILI YA MWAKYEMBE KUA NA ASILI HIYO

    ReplyDelete
  21. IT WAS A CONFLICT OF INTEREST, TOKA MWANZO NILIKUWA NA WASIWASI JUU YA KAMATI YAKE, ALINYIMWA TENDA NDO MAANA AKAKOMALIA REPORT YAKE, WANASIASA WANATAKIWA KUACHA KUFANYA BIASHARA, KAMA WALIVYO WENZETU MAJUU, NA KAMA WANAFANYA WANATAKIWA KUWEKA WAZI JAMANI, TUSIWADANGANYE WALALA HOI NI DHAMBI JAMANI.

    ReplyDelete
  22. NA HAWA NAO ANAOLETA VIGEZO VYA UKABILA WAMETOKA WAPI?
    BADO TU TZ YA SASA INA WACHACHE WANAODHANI UZALENDO WA RAIA HUPIMWA KWA RANGI AU ASILI YAKE?
    SASA NYINYI MTAWAAMBIAJE WAAMERIKA WANAOONGOZWA NA RAIS MWENYE ASILI YA KENYA OBAMA? NA GAVANA SCHWATZENEGGER?
    MBONA HII SI TZ MNAYOIFIKIRIA NYINYI?
    WABAGUZI WAKUBWA!!!
    TULIKUWA NAO HAPA KINA AMIR JAMAL ZAMA ZA AWAMU YA KWANZA, WACHAPA KAZI KULIKO HATA WEUSI WENGI TU, MNAYAJUA HAYO?
    MSIWE NA FIKRA ZILIZODUMAA ZISIZOONA DUNIA ILIPO NA IENDAKO. ASIPIMWE MTU KWA ALIKOTOKA BALI KWA ANACHOKIFANYA. UJASIRI WA ROSTAM NA WENGINE MFANO WAKE, AMBAO ASILI YAO SI TZ LAKINI SASA WAMO KATIKA HARAKATI ZA SIASA NI ZA KUPONGEZWA SANA SANA. NA KAMA WANAFANYA KOSA LOLOTE BASI WASIHUKUMIWE KWA RANGI AU ASILI YAO.
    HAKUNA SHERIA KWA MUJIBU WA ASILI.
    HUO NI UBAGUZI WA RANGI AMBAO HUKO AFRIKA ULIHALALISHWA NA MAKABURU SAUZI PEKEE.
    JAMAA JIELIMISHENI
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  23. Amesema mwenyewe ana makampuni kibao na hiyo ya power ni moja tu amabyo ni nduuuuuuuuuuchi ambapo an share millioni moja - yaani vijisent tu na wala hatujaanza operation. kwa sasa ni kijimradi tu ka wazalendo maskini hohehae wenye paspport moja tu (sio sawa na wale wenye tatu kama Kiyumba anetoa mpunga na gari nyekundu au Chenga mwenye vijihela visogo tu)

    Sasa hizo kamppuni zake kubwa ni zipi na anamiliki kiasi gani wakati juzi juzi tu alikuwa ana kula chaki Mlimani?

    Sasa ndio tunajua kuwa wakubwa hawatishwi na nyauuuuuu

    ReplyDelete
  24. Mwanzo wa kunukuhu "Alisema kwa sasa wanahitaji mitambo na Sh nusu trilioni, ili wawezekuanza kuzalisha umeme.
    “Kampuni hii ni ya watu masikini hawana fedhani ndoto kuzipata hizo nusu trilioni lakini tunajitahidi" mwisho wa kunukuhu.

    Hii ni mara yangu ya kwanza kusikia mtu anazungumzia interms of trillions. Huko nyuma nilizoea kuona mafisadi lakini walikuwa kwenye billions. I think this is another new level.

    Mtu anazungumza interms of trillions halafu anathubutu kujiita masikini? One trillion ni sufuri kumi na mbili
    1,000,000,000,000
    ambayo ni karibia sawa na dola za kimarekani million 770

    Naomba wenzangu mniambie labda I'm dreaming

    ReplyDelete
  25. Jamanii richmond ni texas.tenende anakaa houston.makubwa

    ReplyDelete
  26. 1:- Tarehe March 20, 2009 1:34 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Nchi imekwisha!!

    Kumbe hata huyu ndivyo alivyo!!!

    Yaani alikuwa mstari wa mbele kukaba Richmond na Dowans wakati yeye mwenyewe ana interest zake katika hiyo sekta.

    Nchi zenye maadili huwzi kupata nafasi ya kuumiza wapinzani wako wa kibiashara kwa kutumia mgongo wa Ubunge.

    Kuna actual and perceived conflict of interests, zote ni ufisadi.

    Kumbe anataka yeye ale!!!

    KUMBE HATA KWENYE BLOG YETU YA JAMII KUNA VIBARAKA WANATUMWA KUTAKA KUPOTOSHA UKWELI DUH... WE ANON ACHA UBABAISHAJI HAPA

    2:- Tarehe March 20, 2009 1:52 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    MUNGU INUSURU TZ.YETU HAAA?HILI MWAKYEMBYE MWEMBWE ZOTE ZILE KUMBE NALO FISADI,
    KWELI KIKWETE JINIAZI KUWATOA NJE WANASIASA NA KUFANYA BIASHARA ALILIJUA HILI KUA UNAFKI UTAKUEPO KTK KUJAJI MASLAHI YA KWELI YA TAIFA
    NYINYI MNAO MTETE MWAKYEMBE KWA UKABILA WENU ACHENI UPUUZI WENU MAANA HAKUNA MTAKACHO FAIDIKA ZAIDI YA BIBI ZENU NA WAJOMBA ZENU NA TAIFA KWA UJUMLA KUWA MASKINI
    UZALENDO HAUTIZAMWI KWA RANGI BALI UZALENDO WA KUTOKUA MNAFKI UIPENDE NCHI KWA DHATI
    MAANA TUKITAKA KUTIZAMA RANGI HUYO MWAKYEMBE ANAWEZA KUA NI MZAMBIA AMA MMALAWI
    ONDOENI UPUZI WENU HAPA KUTETEA WANAFKI WANAOWEKA MASLAHI YAO BINAFSI BADALA YA TAIFA NA KUWADANGANYA WASIO NA ELIMU KAMA NYINYI
    LAKINI HATUWEZI KUSHANGAA KUTOKANA NA ASILI YA MWAKYEMBE KUA NA ASILI HIYO

    wewe na huyo anon hapo juu ndo wale wale kwanza nahisi ni mtu mmoja na si ajabu ukawa kibaraka wa Rostam na umeajiriwa kwenye moja ya magazetyi yake duh, mnatia aibu sasa huu uwanja si wakusafishana bwana ni lazima tusimamie kwenye ukweli hakuna ubabaishaji hapa, soma vizuri alichokisema mwakyembe au kama unaona unapata shida sana kusoma nenda www.jamiiforums.com huko unaweza ukasikia chopte alichokiongea mh Mwakyembe.

    GO MWAKYEMBE GO HAKUNA WA KUKUBABAISHA WEWE NI SHUJAA ULIYEWEKA HISTORIA KWENYE NCHI HII HAKUNA WA KUKUPINGA HATA HAO WANAOSEMA KUWA WEWE NI FISADI WAACHE WAKAE NA UELEWA WAO MDOGO WANACHI TUPO PAMOJA NAWE HATUTAKUBALI KUYUMBISHWA NA ROSTAM KABSAAA NA JIMBOP LAKE KULE LAZIMA ALIKOSE HATA LIKICHUKULIWA NA UPINZANI NA LICHUKULIWE TU KULIKO KUENDELEA KULISHIKILIA HUYU FISADI AMBAYE ANATHAMINI MAMBO YAKE TU NA KUKIMBIZIA PESA ZOTE HUKO KWAO IRAN.

    TANZANIA ITALILIWA NA ITATETEWA NA WAZAWA HALISI SI WAZAWA WA KUCOPPY.

    NI HAYO TU MKUU WA WILAYA

    ReplyDelete
  27. Kumbe Mwakyembe naye ni mtu wa FULANAZ mtindo mmoja. Au Michuzi ilimmegea siri ya mafanikio ya FULANAZ. ENDELEZA LIBENEKE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...