Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
 VIPODOZI ambavyo vimepigwa mrufuku vyenye thamani ya milioni 72,406,500 pamoja na Pombe kali zilizopigwa marufuku zenye thamani ya Sh.Milioni 11,356,000 vimekamatwa vikiwa kwenye maduka wakiuziwa wananchi.

Hayo yamebainiswa leo Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) , Agnes Kijo ,wakati alipokuwa anatoa taarifa kuhusu  ukaguzi maalum wa kukagua na kuondoa katika soko  vipodozi visivyosajiliwa,pombe kali zisizosajiliwa pamoja na kufuatilia uhalali wa biashara ya vipodozi kwenye mitandao ya kijamii.

Kijo ameseka katika ukaguzi huo ambao ulishirikisha Jeshi la Polisi,TFDA,Shirika la Viwango nchini (TBS),Wakala  wa Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na Ofisi ya Rais,

Amesema katika ukaguzi huo walifanya katika mikoa ya Dar es Salaam,Pwani,Mwanza,Shinyanga,Geita,Mara na Arusha ambapo ukaguzi huo ulichukua mda wa siku mbili.

Kijo amevitaja vipodozi vilivyokamatwa ni Carolight cream,Citrolight Crem,Sivoclaire Cream,Max light cream,dawa zinazodaiwa kuongeza maumbile kwa wanaume(Maxman capsules) sabani za kurudisha usichana ( Virginity soap).

Vipodozi vengine ni Dawa za kuongoeza ukubwa wa maziwa kwa wanawake (Papaya breast enlarging crem) pamoja na dawa za kutibu magonjwa ambazo zimekuwa zikitumika kimakosa.

Sanjari na Vipodozi hivyo vilivyopigwa marufuku pia katika ukaguzi huo wamekatamata  pombe kali zenye ujazo milimita 200  ambazo  zinazofungaswa kwenye viroba.

"Tumekamata pombe hizi ni imperial blue whsky,White mischief vodka,contessa preimium dry gin vodka,Konyagi (Ladha ya pesheni)magic movement vodka,officers choice ,Dewer's white label,Officers can spirit,sinature vodk "amesema Kijo.

Hata hivyo Kijo amesema baada ya ukaguzi huo wamechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufunga majadala 24 ya kesi katika vituo vya  Polisi dhidi ya watuhumiwa  na majengo ya biashara 29 yamefungwa.

"Baada ya uchunguzi wa makosa kukamilika hatua za kisheria zinatachukuliwa ikiwa pamoja na kuwapeleka mhakamani watuhumiwa na kutoa dhabu kulingana na sheria ya Chakula,Dawa na Vipodozi ,Sura  219.Adhabu hizo zinajumuisha kufutwa leseni ya biashara na kuharibu bidhaa zilizokamatwa kwa gharama ya mtuhimiwa,"amesema

Kijo amewataka wananchi kuendendelea kutoa taarifa za wale wote wanaojihusisha na biashara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku ,Biashara harany ya vipodozi na dawa katika mitandao ya kijamii ili hatua zichukuliwe na Mamlaka husika.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na operesheni walioifanya hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...