KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhandisi Steven Daudi Malekela Mlote kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chai Tanzania (Tea Board of Tanzania – TBT).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Steven Daudi Malekela Mlote umeanza tarehe 21 Mei, 2018.
Mhandisi Steven Daudi Malekela Mlote anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Geofrey Suleiman Mkamilo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Research Institute – TARI).
Uteuzi wa Dkt. Geofrey Suleiman Mkamilo umeanza tarehe 22 Mei, 2018 na kabla ya uteuzi huu, alikuwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Mashariki, Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ilonga Mkoani Morogoro.
Dkt. Geofrey Suleiman Mkamilo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fidelis Angelo Myaka ambaye amestaafu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

23 Mei, 2018

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...