Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (katikati) akikabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Beki ya CRDB, Dk. Charles Kimei mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mia mbili na arobanini (240 mil) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bungando, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ukarabati na upanuzi wa Jengo la Huduma za wagonjwa wa dharula (Emergency Medicine Department) katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dkt. Abel Makubi na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akitoka hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Beki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, katika hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mia mbili na arobanini (240 mil) kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ukarabati na upanuzi wa Jengo la Huduma za wagonjwa wa dharula (Emergency Medicine Department) katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bungando, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi akizungumza machache wakati akitoa shukrani kwa Uongozi wa Benki ya CRDB, kwa msaada wa shilingi milioni mia mbili na arobanini (240 mil) kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ukarabati na upanuzi wa Jengo la Huduma za wagonjwa wa dharula (Emergency Medicine Department) katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dkt. Abel Makubi (kushoto) akimueleza jambo Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (koti jeusi) aliyeambatana na baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo pindi walipotembelea sehemu ya Jengo la Huduma za wagonjwa wa dharula (Emergency Medicine Department) inayofanyiwa ukarabati katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018. Wengine pichani ni baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB pamoja na Uongozi wa Hospitali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...