Na Rhoda Ezekiel, Kigoma 

WANAFUNZI 346 wa kidato cha kwanza katika Wilaya Kakonko mkoani Kigoma ambao walikuwa hawajaanza masomo kutokana na shule walizopangiwa kuwa na uhaba wa madarasa wanatarajia kuanza masomo mwishoni mwa Aprili mwaka huu.

Hatua hiyo inatokana na jitihada za Serikali wilayani humo kuhakikisha wanafunzi waliofaulu na kutakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wanakwenda shuleni.

Akizungumza hivi karibuni Ofisa elimu kwa Shule za Sekondari wilaani hapa Christopha Bukombe amesema miongoni mwa wanafunzi 1,714 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza walishindwa kuripoti ni 346 waliopangiwa katika shule ya Kanyonza, Muhange na Gwanumpu.
Bukombe ametoa takwimu hizo baada ya kupokea msaada wa mifuko ya saruji na mabati 60 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa vitano na baada ya mwezi huu kuisha wanafunzi watajiunga kutokana na changamoto kutatuliwa.

Amesema katika shule ya Kanyonza kuna wanafunzi 78, Muhange 97 na Gwanumpu 171 ambapo kutokana na upungufu huo walianza kuhamasisha wananchi kuchangia na Serikali imetoa Sh.milioni 8 katika shule mbili za Kanyonza na Gwanumpu na Sh.milioni 4 kwa shule ya Muhange.

Mchango huo wa umetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa lengo la kutatua changamoto hiyo na wanafunzi wataanza masomo kwani walichokuwa wanasubiri fedha kutoka Serikalini.Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amekabidhi saruji na mabati hayo kwa lengo la kuunga mkono jitihada za wananchi ambazo wamezionesha.

Amewapongeza watendaji wa kijiji, madiwani na wenyeviti wa vijiji kwa jitihada zao kubwa katika kufanikisha ujenzi wa madarasa ili wanafunzi wapate elimu.Amesema Serikali inatamani kuona kila mtoto anapata elimu na ni jukumu la wazazi kujitoa ili kutatua baadhi ya changamoto zinazo jitokeza, kwani Serikali haiwezi kufanya kila kitu.
"Niwaombe wananchi mnapoambiwa elimu bila malipo si kwamba hata kujitolea kwenye ujenzi mshindwe, watoto ni wa kwenu lazima mnapoona Serikali haijakamilisha jambo fulani mfanye wenyewe suala hili ni letu sote.

"Lazima wanafunzi wote wapate elimu ni haki yao hakuna urithi mwingine tutakao waachia watoto wetu zaidi ya elimu lazima mtambue kuna michango mingine Wananchi wanatakiwa kuchangia kuhakikisha changamoto hizi zinakwisha,"amesema Kanali Ndagala.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Gwanumpu, Toy Butono amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutoa msaada huo na kuwaomba wananchi kuendelea kuchangia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...