Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege amewataka wauzaji, waagizaji, wasambazaji na wadau wote wa dawa pamoja na Vifaa Tiba Nchini kuchangamkia fursa inayotolewa na Serikali ya kuwa Mshitiri mteule ‘Prime Vendor’ kusaidia katika utoaji wa dawa katika Mikoa yote Tanzania. 
Kandege ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Wadau wa dawa  ‘Vendors Forum’ kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na wadau wa Afya ‘HPSS’ chenye lengo la kuweka uelewa wa pamoja kuhusu uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo wa Mshitiri.
Amesema “mfumo huu utatumika kupata mahitaji ya bidhaa za Afya pale ambapo vituo vya kutolea huduma za Afya vya Umma vitakosa au kupata kiwango pungufu toka Bohari Kuu ya Dawa na pia utasaidia kupunguza kero za Afya ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya”.
Sasa basi ninyi kama wazabuni muhimu katika sekta hii ya Afya wenye Uzalendo na nia njema na Nchi ya Tanzania mnatakiwa kujitokeza katika mchakato wa kumpata Mshitiri (Prime Vendor) wa kila Mkoa ambaye atakidhi vigezo kwa mujibu wa taratibu manunuzi alisema Mhe. Kandege.
Wakati huo huo Naibu Waziri Kandege aliwafahamisha wadau wa dawa kuwa Serikali imagatua mipango na bajeti kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya na inapeleka Fedha moja kwa moja kwenye akaunti za benki zilizofunguliwa katika kila kituo hii itasaidia katika kufanya manunuzi ya dawa hizo na kurahisha mchakato wa malipo. 
“Hivyo niwahakikishie kuwa utaratibu wa malipo utakua ni rahisi na wa haraka zaidi kwa kuwa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati husika zitahusika kuagiza dawa kwa Mshitiri pale mahitaji ya dawa hizo zitakapokosekana kutoka MSD” alisema Mhe. Kandege.
Alimalizia kwa kuwataka Wadau wote wa Dawa kutumia kikao hiki kuelewa kwa undani kuhusu utaratibu huu na kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kumpata Mshitiri Mteule kwani zoezi hili litaendeshwa kwa uwazi na kwa usindani mkubwa.

  Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege(mbele) akifungua kikao cha wadau wa Afya ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika Ukumbi wa Dodoma Hotel.
Mkurugenzi wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi, Dr. Ntuli Kapologwe akitoa maelezo ya awali kabla hajamkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha wadau wa Afya Vendor Forum.
 Mfamasia Mwandamizi  toka Ofisi ya Rais Tamisemi, Regina Richard akielezea malengo la kikao cha Wadau wa Dawa ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel mapema.
  Wataalam toka Idara ya Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau wa Dawa wakiwa katika kikao maalum cha wadau wa dawa.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege(mbele katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu na wadau wa dawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...