Na Hamza Temba-Dodoma

Serikali imefanikiwa kudhibiti vitendo vya ujangili hapa nchini kwa zaidi ya asilimia 50.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.Dk. Kigwangalla alisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita hakuna mauaji mapya ya wanyamapori yaliyoripotiwa na kwamba nyara zinazokamatwa hivi sasa ikiwemo meno ya tembo na ngozi za wanyamapori ni masalia ya zamani.

Amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kudhibiti vitendo vya ujangili ikiwemo doria za mara kwa mara za kiitelijensia ambazo zimekuwa zikishirikisha vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na raia wema. 

Alisema Serikali itaendelea kudhibiti vitendo hivyo kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo ya hifadhi nchini ikiwa ni pamoja na kuanzisha jeshi maalum la usimamizi wa Misitu na Wanyamapori, Sheria ya wanyamapori na za taasisi za uhifadhi zimeanza kufanyiwa marekebisho kuwezesha mabadiliko hayo.

Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla amemueleza balozi Cooke kuwa, Serikali kupitia Wizara yake inaendelea kuimarisha  vivutio vya utalii hapa nchini kwa kupanua jeografia ya maeneo ya utalii sambamba na kuongeza vivutio ili kuongeza idadi ya watalii na mapato.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na msafara wa balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...