JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

               20 KIVUKONI FRONT,
                          P.O. BOX 9000,
                 11466 DAR ES SALAAM,  
                                   Tanzania.


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za mafunzo ya muda mrefu kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika yatakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Pan African (PAU).
Mafunzo hayo ambayo yapo kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu yatatolewa katika kozi mbalimbali zikiwemo Baiolojia, Hesabu, Uhandisi, Sayansi ya Afya, Usimamizi wa Mazingira, Sayansi ya Michezo, Mifugo, Uongozi na Mtangamano, Lugha, Ukalimani wa Mikutano na Ufasiri, Uhandisi wa Maji na Nishati.  
Kwa waombaji wa Shahada ya Uzamili wanatakiwa kuwa na  miaka isiyozidi 30 kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 35 kwa waombaji wanawake. Aidha, kwa waombaji wa Shahada ya Uzamivu wasiwe na miaka zaidi ya 35 kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 40 kwa waombaji wanawake.
Maombi ya mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao (online) kupitia anuani ya barua pepe ya pau-au.net. Mwisho wa kutuma maombi ya fursa hizi ni tarehe 20 Aprili, 2018. Maelezo ya ziada kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia pau.scholarships@africa-union.org au www.pau-au.net. Mratibu wa Mafunzo haya ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...