Upatikanaji wa maji mijini na vijijini umeimarika kutoka chini ya 50% ya awali kutokana na umakini katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji safi nchini. Aidha, ili kukabiliana na mazingira Serikali imeanza mchakato wa kutumia mifumo ya kisayansi ili kuondoa matumizi ya mkaa majumbani.
Hatua hizo zimebainishwa na Mhe. Isack Kamwelwe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira) walipokuwa wakieleza utekelezaji wa hoja za CAG katika sekta zao.
Akizungumzia hoja kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji nchini, Waziri Kamwelwe amesisitiza kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, ufuatiliaji na kuzibwa mianya ya ubadhirifu vimeleta mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini.
“Sisi kwa upande wetu CAG anatuonesha njia ili tufanye vizuri zaidi. Hadi kufikia Desemba, 2017, upatikanaji wa maji mijini umepanda hadi kufikia asilimia 78. Kwa upande wa vijijini, hadi kufikia Machi 2018, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imejenga vituo vya kuchotea maji 123,888 vyenye uwezo wa kuhudumia takribani watu milioni 30 sawa na asilimia 68.8,” alisema.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu hoja mbalimbali
zilizobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) katika Wizara yake mapema mjini Dodoma wakati wa
mkutano na waandishi wa habari ( hawapo pichani).
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba akijibu hoja mbalimnbali zilizobainishwa katika ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Ofisi hiyo
mapema mjini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo
pichani).
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa
Mawaziri wote kukutana na waandishi wa habari kujibu hoja mbalimbali
zilizobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) katika Wizara zao mapema mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso
mapema mjini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari
uliowashirikisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
January Makamba. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...