NYOTA wa muziki wa singeli nchini, Suleiman Jabir 'Msaga Sumu', amesema anashukuru kwa kupata shoo katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga, akisema kuwa anakwenda kwa watu wake wa nguvu kutokana na kufahamu kuwa wanaupenda muziki wake.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Msaga Sumu anayetamba katika muziki huo alisema kuwa wilaya la Handeni ni kati ya maeneo yaliyoupaisha muziki wake, simu chache baada ya kuibuka kwenye tasnia hiyo kutokana na watu wengi wakiwamo waendesha bodaboda waliokuwa wameziweka nyimbo zake kwenye vyombo vyao vya usafiri na kuzicheza muda wote.

Alisema hivyo shoo mbili alizopata kwa kuanzia Jumamosi ya Machi 24 asubuhi hadi jioni kwenye uwanja wa Mabatini, Mkata, wilayani Handeni pamoja na ile itakayofanyika usiku katika siku hiyo hiyo kwenye Ukumbi wa Rombo Hotel kwa kushirikiana na bendi ya Twanga Pepeta, ni sehemu ya kwenda kutuliza kiu ya mashabiki wake wa muziki wilayani humo, mkoani Tanga.

"Handeni nitaanza Mkata kwenye uzinduzi wa ligi ya Handeni Kwetu Cup Machi 24 na baadae nitakuwapo Rombo Hotel, Handeni Mjini, nikiamini ni sehemu nzuri kwangu kutokana na nguvu ya mashabiki wangu kwa namna moja ama nyingine.

" Ni watu wa nguvu kwasababu wanaupenda sana muziki wangu, ukizingatia kuwa mimi msanii hivyo napaswa kufahamu mahala gani nakubalika ili kuhakikisha kuwa nalinda tbamani yao kwangu kama njia ya kuendelea kuniletea mafanikio katika kona ya muziki wa singeli ambao bila kuficha mimi ndio mfalme wao kutokana na uwezo wangu kimuziki,"Alisema Msaga Sumu.

Msaga Sumu anayetamba pia na nyimbo ya Mwanaume Mashine, Shemeji na nyinginezo, alitumia muda huo kuwataka mashabiki wake kuingia kwa wingi kwenye maonyesho mawili ya uzinduzi wa ligi ya Handeni Kwetu Cup Mkata na lile la Rombo Hotel, ili wajionee mambo mapya kutoka kwake.

Ligi ya Handeni Kwetu Cup inaanzishwa na mdau wa michezo Kambi Mbwana, huku ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi Machi 24 na kufikia ukingoni mwezi Oktoba mwaka huu, huku ikishirikisha timu mbalimbali za wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...