Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii 

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita amewasilisha mpango wa Bajeti wa mwaka 2018 hadi 2019 ambapo jumla ya Sh. bilioni 75.2 zitatumika kwa mwaka huo katika shughuli mbalimbali.

Baada ya kuuwasilisha mpango huo kwenye Baraza la Madiwani umepitishwa kwa kauli moja na madiwani hao huku wakipongeza kuwa Jiji la Dar es Salaam limepata Meya anayejali maslahi ya wananchi wa Jiji hilo.

Akizungumza alipokuwa akiwasilisha Mpango huo wa bajeti,Mwita amesema Halmashauri hiyo imeandaa mpango huo kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa kufuatwa na mamlaka za Serikali za mitaa katika utayarishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha wa 2018 na 2019.

Amefafanua Jiji linatarajia kukusanya na kutumia Sh. bilioni 75.2 itakayotokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo Sh.bilioni 18.1 ambazo zinatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye vyanzo vya vyandani.

"Mapato mengine yatapatikana kutokana na halmashauri kubuni vyanzo vingine vya mapato sambamba na kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa mapato." Utekelezaji wa bajeti hiyo umelenga kutekelaza mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis,kuboresha miundombinu ya Dampo,ujenzi wa vyoo vya Umma na kuhakikisha utoaji wa huduma usiokua na usumbufu kwa wananchi,"amesema Mwita.

Ameongeza Jiji la Dar es Salaam limepanga kutumia asilimia 65 ya mapato ya ndani sawa na Sh.bilioni 11.7 kwa ajili ya kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo huku Sh. bilioni 1.08 zitatumika kwa ajili ya mfuko wa wanawake ,vijana na wal

Kuhusu utalii,Mwita amesema kwenye bajeti hiyo zaidi ya Sh.bilioni mbili zimetengwa kuboresha sekta ya hiyo ikiwemo kununua mabasi ,kutengeneza na kuboresha vivutio mbalimbali vilipo jijini hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...