Wananchi mkoani Mara
wamejitokeza kwa wingi kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa Mhe. Adam Kighoma Ali Malima
ambaye amewataka wakazi wote wa mkoa huo kuhakikisha wanasajiliwa Vitambulisho
vya Taifa ndani ya miezi mitatu ya zoezi hilo linaloendelea katika Wilaya zote
za mkoa huo.
Akizungumzia mwitikio wa
wananchi katika kutekeleza agizo hilo; Afisa Usajili Wilaya ya Musoma Bi. Ohana
Gerald amesema mwitikio mkubwa wa watu ndiyo umepelekea kwa Wilaya ya Musoma Manispaa;
zoezi la usajili kuwa limekamilika na
sasa zoezi linaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini na tayari
Kata za Bwasi, Makojo na Bukumi
zimemaliza Usajili. Kata zinazoendelea na usajili kwa sasa ni Bukima, Suguti na
Rusoli.
Aidha amewataka wananchi wa
kata nyingine 15 ambazo bado usajili haujaanza kuanza maandalizi na kujitokeza
kwa wingi pindi zoezi litakapofika katika kata zao.
Baadhi ya wananchi
wameonyesha uelewa mpana wa manufaa ya kuwa na Vitambulisho vya Taifa na
kuishukuru Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuendesha zoezi
bila kulipia gharama zozote.
Pamoja na kuisifu Serikali
wamemshukuru Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima kwa kuweka msukumo mkubwa wa
zoezi la Usajili kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakinyanyasika kwa
kukosa utambulisho na hivyo kukosa fursa nyingi na kuwapunguzia kero na usumbufu
mkubwa wanaoupata sasa katika kupata baadhi ya huduma.
Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa inategemea kumaliza zoezi la Usajili kwa mkoa wa Mara mwishoni mwa mwezi
Februari, 2018 na kuendelea na hatua za uchakataji wa taarifa ili kuhakikisha
wananchi wote wenye sifa waliosajiliwa mkoani Mara wanapatiwa Utambulisho wa
Taifa kabla ya mwezi Desemba 2018.
Wakazi wa kata ya Bukima Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara, wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.
Mwenyekiti wa kijiji cha Bukima Ndg. Murungu Murungu akiwasaidia wananchi kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi la Usajili likiendelea kwenye ofisi ya mtendaji kata ya Bukima.
Afisa usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi. Ohana Gerald akimsikiliza mmoja wa wananchi waliojitokeza kusajiliwa wakati wa zoezi la usajili wananchi wa kata ya Bukima wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara.
Bw. Shukrani Kwikalya Mgane mkazi wa kata ya Bukima, akikamilisha hatua ya upigaji wa picha wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa. Kulia ni afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bw. Jackson Paulo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...