Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
Mahakama ya wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemuhukumu Mwalimu wa Sanaa ya kujihami, 'Martial arts' Salum Njwete maarufu kama Scorpion, kutumikia kifungo cha miaka saba gerezani na fidia ya sh. Milioni thelathini ambayo anatakiwa haraka iwekenavyo.
Hukumu hiyo imesomwa baada ya Scorpion kupatikana na hatia katika kesi ya kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho kinyozi Said Mrisho na kuachiwa huru kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.
Hukumu dhidi ya Njwete ambaye pia ni msanii wa filamu za kibongo na mshindi wa shindano la Dume Challenge ambapo alijinyakulia kitita cha milioni 20 imesomwa na Hakimu Mkazi Wa mahakama hiyo Flora Haule.
Salum Njwete maarufu kama "Scorpion"  akitolewa mahakamani leo mara baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho kinyozi Said Mrisho leo kwenye mahakama ya Ilala jijini Dar es Salaam. Picha na Mudy wa Blogu ya Jamii
 Said Mrisho(aliyevaa miwani) akitoka mahakamani leo mara baada ya hukumu kutolewa leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...