Na Mwamvua Mwinyi-Bagamoyo
NAIBU Waziri Wa Nishati Subira Mgalu, ameridhishwa na kasi na kazi anayoendelea nayo mkandarasi wa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya III Sengerema huko kijiji cha Kongo na kata ya Yombo wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Aidha amelitaka shirika la umeme (Tanesco) wilaya ya Bagamoyo, kukimbizana na wakati kwa kuwapa wananchi fomu za kujaza ili kupatiwa umeme wakati zoezi la kuweka nguzo likiendelea katika baadhi ya vijiji.

Aliyasema hayo wakati alipokwenda kutembelea kijiji cha Kongo ,kata ya Yombo na Visezi kata ya Vigwaza na kujiridhisha na kazi ya mradi huo inavyoendelea .Mgalu alisema mkandarasi huyo ameahidi kumaliza kazi hiyo mwanzoni mwa mwezi ujao na kwa uhakika anakwenda vizuri.

Alieleza kwasasa amekuta wanaendelea na kazi ya kusimamisha nguzo na maeneo mengine yanatarajiwa kutandaza nyaya ."Mkandarasi Sengerema yupo Mkoa wa Iringa na Pwani ,ameanza kazi vizuri na ndivyo tunavyohitaji ,tunaomba aendelee na kasi hii ili wananchi wapate huduma hii ya umeme haraka" alisisitiza Mgalu.
Naibu waziri huyo,alitoa tahadhali kwa wakandarasi wengine wa mradi wa REA kwenda na kasi inayotakiwa na serikali ya awamu ya tano,na atakaefanya kazi chini ya kiwango hatakuwa na masihala nae.
 Naibu Waziri Wa Nishati  Mhe. Subira Mgalu mwenye kitambaa chekundu kichwani  akiwa ameambatana na mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa wa pili kushoto na wengine ni viongozi mbalimbali wa kijiji cha Kongo na kata ya Yombo wakati alipokwenda kutembelea maeneo yanayotekelezwa mradi wa umeme vijijini (REA )awamu ya III ,ambapo amejiridhisha na kasi anayoendelea nayo mkandarasi Sengerema.

 Nguzo 60 za umeme zilizotelekezwa ndani ya miaka mitatu huko kijiji cha Visezi Kata ya Vigwaza pasipo kufanyiwa kazi ,jambo linaloelezwa ni uzembe uliofanywa na mkandarasi MBH aliyepewa kazi awamu ya pili ya mradi wa umeme vijijini (REA )ambapo ameitia hasara serikali na kuchelewesha huduma ya umeme kwa jamii.
Naibu Waziri Wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Visezi kata ya Vigwaza kuhusiana na masuala ya huduma ya umeme.
 Mbunge wa jimbo la Chalinze  Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo kuhusiana na changamoto ya nishati ya umeme huko kijiji cha Visezi kata ya Vigwaza. Picha na  Mwamvua Mwinyi

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...