NaJoel Maduka-Geita.

Jumla ya Sh Bilioni 3 zilizotolewa na serikali Mkoani Geita zinatarajiwa kuboresha miundombinu katika Vituo saba vya afya .

Mganga mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt Japhet Simeo alisema lengo kuu la hizo fedha ni kuboresha miundo mbinu kwa maana ya chumba cha upasuaji kujenga wodi ya watoto,wakina mama ,maabara na chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba wanatarajia kuona fedha hizo zinafanyika kuboresha mandhari ya kituo kwa maana ya bustani na majengo ambayo yamechakaa.

Simeo alizitaja wilaya ambazo zimepatiwa fedha hizo ni wilaya 5 ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Geita ambayo imepewa kiasi cha sh ,Milioni 500 kwenye kituo cha afya cha Nzera na kwamba hadi sasa wameshajenga majengo manne ambayo yamekaribia kukamilika , Mbogwe milioni 800 ambazo zimegawa kwenye vituo viwili vya afya, Bukombe milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha uyovu , Chato wamepatiwa fedha kwaajili ya vituo viwili ambvyo ni Bwanga Milioni 500 na Karumwa milioni 400 na Wilaya ya Nyang’hale milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha Nyang’hale.

Juma Mabura ni moja kati ya wananchi wa Wilaya ya Mbongwe ambapo ameelezea kuwa kumekuwape na changamoto kubwa ya upungufu wa majengo na kwamba kukamilika kwa baadhi ya majengo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma ya afya.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa majengo yaliyo kwenye hatua ya renta na maboma yakikamilika watakuwa kwenye asilimia 55 kwa maana ya zahanati 262 na kwamba nyingine wameanza ujenzi .

Aidha amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuondoa kero ya kimiundombinu kwenye sekta ya afya ili kuwawezesha watanzania kupata huduma bora za afya.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki kuchimba msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. 
Wananchi wakishiriki kwenye ujenzi wa msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. 
Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe ,Mathar Mkupasi akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kuunga mkono jitihada za serikali za ujenzi wa jengo la kupasulia kwenye kituo cha afya cha Masumbwe. 
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM,Wilayani Mbongwe Johari Juma akisisitiza wanachama wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kushiriki katika shughuli za maendeleo. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza namna serikali ilivyojipanga kupunguza changamoto ya huduma za afya Mkoani humo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mbongwe. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...