Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu toka kulia leo
asubuhi alishiriki mazoezi ya utayari na kuwatia hamasa Askari wa Mkoa
wa Tabora, katika ziara yake ya siku moja mkoani humo, hatua hiyo ni
kutokana na kuwataka askari wa Jeshi la Polisi kuwa na utayari wakati
wote.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiwa amembeba Joshua
mtoto wa muumini wa kanisa la Siroham mkoani Tabora kabla ya uzinduzi
wa zahanati ya Polisi iliyojengwa kwa hisani ya kanisa hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu kutoka kushoto
akiangalia mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi akiwa katika mazoezi ya
utayari kupita juu ya kamba mkoani Tabora leo. Picha na Jeshi la Polisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...