Kaimu Mkurugenzi masuala ya wateja wa Mamlaka ya udhibitiwa huduma wa nishati na maji(ZURA) Mussa Ramadhani Haji akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini Maisara Zanzibar.(Picha na Kijakazi Abdalla Maelezo Zanzibar.)

MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Zanzibar (ZURA) imetoa taarifa juu ya bei mpya ya mafuta itakayoanza kutumika rasmi kuanzia kesho Jumanne tarehe 12-12-2017. Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Maisara, Kaimu Mkurugenzi masuala ya wateja, Mussa Ramadhani Haji  alisema kuwa bei hizo Zura imepanga kufuatia mambo yafuatayo;-

Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations) katika mwezi wa Novemba 2017 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanyia mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi wa Disemba 2017.

Pia thamani ya shillingi ya  Tanzania , gharama za usafiri , Bima na’ Premium ‘hadi Zanzibar  . Kodi za serikali  na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

Alisema bei za rejereja ya mafuta ya Petroli kwa mwezi wa Disemba, 2017 imepanda kwa shillingi (100) kwa lita kutoka shilling 2,130 Mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 2,230 kwa lita katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.5%.

Pia alisema bei ya rejereja ya mafuta ya Dizeli kwa Mwezi wa Disemba , 2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shilling 2,280 kwa lita katika mwezi Novemba hadi shilling 2,190 kwa lita katika mwezi wa Disemba, 2017 sawa na  asilimia 4%.

Aidha alisema bei ya reja reja ya mafuta ya Taa kwa mwezi wa Disemb 2017 imepanda kwa shilling (80)  kwa lita kutoka shillingi 1.539 kwa lita katika mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 1,619 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.9%

Vilevile bei ya reja reja ya mafuta ya Banka kwa mwezi waDisemba,  2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shillingi 2,122 kwa lita katika mwezi wa Novemba, 2017 hadi shilling 2,032 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.4%.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...