Makocha 28 wanawake kutoka vyuo mbalimbali vya Maendeleo ya Jamii nchini leo Oktoba 17, 2017 wamehitimu kozi fupi ya ukocha katika kozi iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO). 

Kozi hiyo ya siku mbili ambayo ni ya pili kufanyika kwa makocha hao, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume - Makao Makuu ya TFF ilikuwa chini ya mkufunzi wa TFF, Raymond Gweba. 

Akizungumza kwenye ufungaji wa kozi hiyo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo amesema Serikali inafahamu kuwa inatakiwa kuwekeza kwenye soka la wanawake kuanzia upande wa vijana na ndio maana inatengeneza mazingira na sera zitakazowezesha mafanikio hayo. 

Singo amesema nchi mbalimbali wana maendeleo makubwa katika mpira wa miguu kwa wanawake na sasa wakati wa Tanzania kuwekeza katika upande huo kuanzia kwa watoto na makocha. 
Wahitimu wa kozi ya Ukocha kwa wanawake wakiwa katika picha ya pamoja Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (katikati) na viongozi wengine kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na Chama cha Soka la Wanawake Nchini (TWFA) pamoja na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO). 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (kushoto) akiwa anamsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi wakati wa ufungaji wa kozi ya wanawake iliyoendeshwa kwa muda wa siku 2, kulia ni Ulf Kjellstig na Mwenyekiti wa soka la wanawake (TWFA) Amina Karuma. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo akikabidhi cheti na vifaa vya michezo kwa moja ya washiriki wa kozi ya ukocha kwa wanawake leo Jijini Dar es Salaam, sambamba na Mwenyekiti wa Soka la wanawake (TWFA) Amina Karuma Ulf Kjellistig. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...