NA ESTOM SANGA- MISUNGWI

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa wa Ireland bwana Ciar`an Cannon T.D amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za jamii na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wananchi hususani wanaokabiliwa na umaskini .

Bwana Ciar`an ametoa pongezi hizo alipofanya ziara katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ambako amekutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na kupata ushuhuda wa namna walivyonufaika na Mpango huo.

Baadhi ya Wananchi wanaonufaika na huduma za TASAF wamemweleza waziri huyo kuwa tangu waorodheshwe kwenye Mpango wameboresha maisha yao kwa huku wakijengewa misingi ya kujitegemea kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi,kuboresha na makazi yao .

Aidha baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wameeleza kuwa wamepata mafanikio makubwa katika sekta ya elimu na afya katika kaya zao baada ya kujiunga na Mfuko wa Afya Jamii kwa kutumia fedha walizozipata kutoka TASAF na hivyo kuwapungizia mzigo mkubwa wa matibabu katika kipindi cha mwaka mzima,jambo ambalo wamesema limeboresha afya zao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga akitoa maelezo kwa waziri wa Mambo ya nje wa Ireland namna shughuli za kuhawilisha fedha zinavyotekelezwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

 Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland akizungumza na Mkurugenzi wa TASAF,Ladislaus Mwamanga  wakati waliposhuhudia zoezi la kulipa ruzuku kwa baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini katika wilaya ya  Misungwi,mkoani Mwanza.

 Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Ciaran akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Misungwi unaotekelezwa na TASAF namna walivyonufaika na huduma za Mpango huo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela (aliyevaa kofia) akiwa na mgeni wake waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland wakiwa na baadhi ya walengwa wa TASAF wakiwa na vyeti vya bima ya afya ya jamii waliyopata baada ya kujiunga na bima hiyo kwa kutumia  sehemu ya ruzuku ya  TASAF.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...