Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Daktari bingwa Wa magonjwa ya moyo wa Hospital ya Aga Khan, Prof. Mustapha Bapunia (62), ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, inashangaza, Manji katika umri mdogo alionao anamatatizo sugu ya moyo ambayo yanampasa kujilinda sana.

Dkt, huyo ambaye ni shahidi Wa tatu upande wa utetezi katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili mfanyabiashara Yusufu Manji amedai hayo leo wakati àkitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.Akiongozwà na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula, shahidi Hugo amedai, Manji ana vyuma vinne kwenye moyo ni hatari na kwamba ni lazima ajiangalie sana kwasababu anaweza kufa muda wowote.

Amedai katika umri mdogo alionao Manji kuwa na vyuma vinne kwenye moyo inashangaza sana na kitaalamy anapaswa kujiangalia sana.Amedai Februari mwaka huu Manji alipelekwa hospitalini hapo akiwa anasumbuliwa na maumivu kwenye moyo ambapo kutokana na historia ya ugonjwa iliyotolewa na manji mwenyewe na kwamba aliwahi kuzibuliwa mishipa ya moyo mitatu ilizibuliwa India, Dubai na Marekani lakini pia bado alikuwa akipata maumivu inaonyesha kuwa anatatizo sugu la moyo.

Alidai kuwa hata baada ya kumfanyiwa uchunguzi ilionekana kuna mshipa mwingine ulioziba licha ya ile iliyozibuliwa kuwa wazi lakini walipotaka kumzibua alikataa na kuomba apewe dawa kwasababu familia yake na matibabu yake yapo marekani.

Baada ya vipimo walimshauriwa kutumia dawa za aina nne ambazo ni muhimu sana kwasababu ya umri wake mdogo ili ya kupunguza maumivu makali. Kwani vipimo vinaonyesha Manji ana maumivu sugu ya mgongo na kukosa usingizi ambapo alipewa dawa za kupunguza maumivu (Benzodiazepines)ambazo zinatotewa kwa cheti cha daktari lakini baadae tatizo lilijirudia na kurudishwa tena february 24,2017 saa mbili usiku ambapo majibu ya vipimo vilionyesha kapata mshtuko, wakarekebisha na kumuwekea chuma na kuruhusiwa Machi 14,2017.
Mshtakiwa Yusuph Manji anayekabiliwa na shtaka la matumizi ya dawa za kulevya, akijadili jambo na Wakili wake Hajra Mungula kabla ya kupanda kizimbani kwa ajili ya kuanza kujitetea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...