Benki ya KCB Tanzania leo imetangaza rasmi udhamini mwenza wa ligi ya soka ya TFF Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi za kitanzania 325,000,000. Mkataba wa makubaliano hayo ulisainiwa rasmi leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na Raisi WA TFF Wallace Karia.

Hafla hiyo ya makubaliano ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya KCB Tanzania, Bi, Zuhura Muro, Mwenyekiti wa bodi  ya Udhamini TFF, Mhe, Mohammed Abdulaziz, Wakurugenzi wa Bodi ya KCB Tanzania, Wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania, wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario alisema kuwa udhamini huo upo ndani ya vipaumbele vya benki kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo. “Sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na pia ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi nchini, hivyo benki ya KCB imechukua uamuzi huu kujiunga na TFF kukuza mchezo wa mpira wa miguu” alisema Kimario.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Zuhuru Muro alisema kuwa “Benki ya KCB Tanzania tunajivunia kuwa sehemu ya ligi hii na tunaamini kuwa udhamini wetu utachangia kuleta hamasa kubwa kwa wapenzi wa mpira wa miguu na kukuza vipaji vya vijana.” Alieleza kuwa udhamini huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa benki, wateja wake, TFF, wachezaji, mashabiki na wananchi kwa ujumla.



Rais wa TFF aliishukuru benki ya KCB kwa kuidhamini Ligi kuu Vodacom jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2017/18. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.


Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (aliyekaa Kulia) na Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia (aliyekaa kushoto) wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi 325,000,000 uliotolewa na benki ya KCB Tanzania kwa TFF. Pamoja nao wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro (aliyesimama kulia), Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura (aliyesimama katikati) na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao (aliyesimama kushoto). 

 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (Katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro (wapili kulia) wakikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 325,000,000 kwa Raisi wa Shirikiso la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia (wapili kushoto), ikiwa ni udhamini kwa ajili ya ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18. Pamoja nao kwenye picha ni Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura (wakwanza Kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao (wakwanza kushoto).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...