Katibu wa Jumuiya ya madola Mhe. Patricia Scotland amefanya mazungumzo na Naibu Waziri Ofisi ya Mkamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga kuhusu suala zima la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira huku eneo la mabadiliko ya Tabianchi likipewa kipaumbele.

Katika mazungumzo hayo Bi. Scotland alisema kuwa kuna kila sababu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuelewa zaidi suala zima la mabadiliko ya tabianchi akieleza kuwa wanasayansi wanasema ifikapo mwaka 2050 dunia inaweza kabisa kuepukana na suala la athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi endapo itawezekana kulifanyia kazi kwa pamoja.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mpina alieleza kuwa Tanzania imeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika sekta mbalimbali na jitihada zimefanyika katika kuwezesha jamii kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema serikali inatekeleza Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi (2012) ambapo sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, nishati zimeandaa na zinatekeleza mpango kazi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Nje ya Ofisi ya Makamu wa Rais Baada ya kumaliza mkutano ulohusu suala zima la usimamizi na Utunzaji wa Mazingira.
Mhe. Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza AshaRose Migiro, akizungumza baada ya kikao na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri Mpina na wataalaam kuhusu masuala ya Mazingira, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na wajumbe walioshiriki mkutano wa masuala ya hifadhi ya mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...