Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam.
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imewaweka chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka miwili Msanii wa Bongofleva Rashid Abdalah maarufu Chidi Benz na wenzake watano baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo dhidi ya maombi hayo.
Aidha, upande wa mashtaka uliwasilisha kiapo hicho kwamba mahakama iwaweke chini ya uangalizi baada ya kubainikia kujihusha na matumizi ya dawa za kulevya.
Maombi hayo yalisikilizwa na kutolewa uamuzi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,Mfawidhi Ritha Tarimo.Mbali na Chidbenzi, wengine watakaokuwa chini ya ungalizi ni, Hadia Abeid, Said Ally, Athuman Elias na Hassan Mohamed.
Wakili wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa upande wa Jamhuri unawasilisha hati ya kiapo kutoka kituo cha polisi Msimbazi kwamba watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya hivyo mahakama itoe dhamana kwani wamekuwa na tabia mbaya katika jamii.
Glory alidai kuwa wanaiomba mahakama itoe amri ya kuwaweka wajibu maombi chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu na kusaidi dhamana ambayo itahakikisha wanakuwa na tabia njema na kutojihusisha vitendo vya dawa za kulevya.
Baaada ya kuwasilishwa kwa maombi hayo, Chidi Benz na wenzake hakuwa na pingamizi.
Akitoa uamuzi hakimu alisema wajibu maombi watakuwa chini ya uangalizi wa polisi miaka miwili na kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaotia saini ya dhamana ya Sh.milioni mbili kila mmoja na kuripoti kituo cha polisi Msimbazi kwa mwezi mara moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...