BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Tanzania, (NEMC), limpongeza mshindi wa droo ya 32 ya Bahati Nasibu ya Biko nchini Tanzania, Edward Gama, mkazi wa Tabata, aliyefanikiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 20 inayotolewa na Biko, huku akitwaa zawadi hiyo katika droo ya Jumatano iliyopita na kumtaka ajihusishe na masuala ya mazingira na ufugaji wa nyuki.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza hilo, Dr Vedast Makota, wakati Gama anapokea hundi yake ya Sh Milioni 20, saa chache kabla ya kukabidhiwa rasmi fedha zake katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam leo (jana).

Akizungumzia ushindi huo wa mwanafunzi anayesubiri ajira, Dr Makota, alisema ni furaha kubwa kwa kijana wao kuibuka na ushindi huo wa Sh Milioni 20 ambapo amekabidhiwa, huku akisema ni fursa kubwa zaidi kama Gama atajihusisha pia na masuala ya mazingira kulingana na taaluma yao.

“Ni furaha kubwa kuona kijana wetu amefanikiwa kuibuka na ushindi huu mnono, hivyo namtaka azitumie vizuri fedha zake pamoja na kuwekeza pia katika sekta ya mazingira ikiwamo ufugaji wa nyuki ambao ni biashara nzuri sana,” Alisema.

Naye Gama aliwapongeza Biko kwa kumkabidhi fedha zake haraka, huku akisema wakati anapokea simu ya Kajala Masanja na Mujuni Sylvester ‘Mpoki’, hakuamini kabisa kulingana na bahati nasibu hiyo inavyohusisha watu wengi wanaocheza Biko kila siku.

Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles mwenye tshirt ya Biko kulia akimkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 Edward Gama kama zawadi yake ya kushinda Biko droo ya 32. Mwenye tshirt nyekundu ni Balozi wa Biko Mujuni Sylvester Mpoki.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...