Waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako alifanya ziara ya ghafla katika shule Mkoani Iringa. Alitembelea shule zinazo fundisha watoto wenye mahitaji maalum za Makala Wilaya ya Mfundi, Shule ya viziwi Mtwivila, Shule ya sekondari ya wasichana Mtwivila na shule ya sekondari ya Lugalo.

 Nia ya ziara hiyo ni pamoja na kukagua vifaa vya kufundishia ambavyo serikali imetoa. Pia alipta fursa ya kusalimia wanafunzi na walimu. Katika ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza, Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Bi wamoja Ayoub, Wakuu wa wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri David na Iringa Mhe.Richard Kasesela. Pia wabunge waheshimiwa, Ritta Kabati, Zainab Mwamwindi na Mch Peter Msigwa​.
Waziri Ndalichako akipokelewa na Mkuu wa wilaya ya Iriga mjini Mh Richard Kasesela pamoja na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mh.Peter Msigwa mara baada ya kuwasili ndani ya Manispaa ya Iringa 
Waziri Prof.Ndalichako  akisikiliza jinsi ya kufundisha watoto wenye ulemavu wa kusikia​.
​Waziri Prof. Ndalichako akiongea na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini,Mhe.Peter Msigwa katika Shule ya Viziwi, Mbunge Viti Maalum Mhe Zainab Mwamwindi akisikiliza​
Waziri  Profesa Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Iringa girls 
picha ya pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum
Waziri Profesa Ndalichako akiongea na wananfunzi wa Shule ya sekondari Lugalo kidato cha 5

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...