Na Lorietha Laurence WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ameridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa eneo la kuchezea mpira (picth) la Uwanja wa Taifa wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza  katika ziara hiyo ya kukagua hatua iliyofikiwa katika matengenezo ya uwanja huo   Waziri  Mhe.Dkt.  Mwakyembe amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya awali ya ukarabati na anatarajia mabadiliko makubwa  zaidi baada ya hatua zinazofuata kukamilika .

 “Nimefurahishwa na mabadiliko niliyoyaona katika hatua hii ya awali naamini ukarabati utakapokamilika milango itakuwa wazi kwa mechi za kimataifa ikiwemo mashindano ya AFCON yanayoratajiwa kufanyika nchini kwetu  mwaka 2019” alisema Dkt.Mwakyembe

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha viwanja vingine vikiwemo vya mikoani  vinafanyiwa ukarabati ili kuboresha sekta ya michezo nchini.

Waziri Dkt. Mwakyembe ameushukuru uongozi wa SPORTPESA kwa kuonyesha ushirikiano wa karibu na Serikali katika kuhakikisha inaweka mchango wake  katika michezo kwa kukarabati sehemu ya kuchezea mpira (picth) ya Uwanja wa Taifa pamoja na vifaa mbalimbali vilivyotolewa katika kuhakikisha kazi hiyo inakamilika.

Naye Mkurugenzi wa Utawala Na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas ameeleza kuwa kampuni yao imefanya hivyo ikiwa ni njia ya kuonyesha uzalendo wa kupenda na kuthamini vya nyumbani.
“Hatua hii ni ya awali baada ya mechi ya Everton na Gorimahiya mnamo Julai 13 mwaka huu  hatua itakayofuata ni ya   kuondoa nyasi zote  na kuotesha mpya ambazo zitachukuwa miezi mitatu kuwa sawa” alisema Bw.Tarimba.

Uwanja wa Taifa ulianza matengenezo ya eneo la kucheze (pitch) rasmi katikati wa mwezi wa sita lengo ni kuhakikisha nyasi zilizochakaa zinaondolewa na kuwekwa nyasi mpya zitazodumu zaidi ya miaka 10 .
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(mwenye miwani) akisikiliza  maelekezo kutoka kwa  Mkurugenzi  Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  Bw. Alex Nkenyenge (wa Tatu kulia) alipotembelea uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge (katikati) alipokuwa akiwatambulisha vijana ambao ni Maafisa kilimo (wenye makoti)  leo Jijini Dar es Salaam , mwingine ni  Mkurugenzi wa Utawala  na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas(mwenye shati jeupe).
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipata maelekezo kuhusu mbegu za nyasi mpya kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius  Mgaya leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea uwanja huo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyeshwa mashine zinazotumika katika ukarabati wa picth katika uwanja wa Taifa kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge (aliyechuchumaa), katikati ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius  Mgaya na kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala  na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas  leo Jijini Dar es Salaam .

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akielezwa jambo kuhusu matumizi    mashine ya kuchorea mistari kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius  Mgaya(aliyeinama) na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge  leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea uwanja huo. picha na Lorietha Laurence WHUSM).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...