Na Khalfan Said
“MANENO ni mawili tu “KA na TA” ukiunganisha Kata, asiyelipa kateni umeme” Hayo yalikuwa ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme mkoani Mtwara miezi michche iliyopita.

Kufuatia maagizo hayo ya Rais, Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wake, Dkt. Tito Mwinuka, aliitisha mkutano na waandihi wa habari na kutoa ilani kwa wadaiwa wote “sugu” wa bili za umeme kuwa walipe madeni yao vinginevyo huduma ya umeme itasitishwa.

Baada ya tangazo hilo, baadhi ya taasisi za serikali likiwemo Jesho la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, naye aliitisha mkutano na wanahabari na kueleza kuwa JWTZ italipa sdeni lake na kuagiza wahusika wafanye hivyo mara moja.

Leo hii Mei 4, 2017, Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, aliwaita waandishi wa habari ofisini kwake na kuwaeleza kuwa taasisi za umma na binafsi zilizo katika mkoa wake, zilikuwa zikidaiwa jumla ya shilingi Bilioni 7, ambapo taasisi za serikali pekee zilikuwa na deni la  shilingi bilioni 6 na kwa sasa tayari zimelipa jumla ya shilingi bilioni 2 na kubaki deni la shilingi bikioni 4.

“Hizi taasisi za umma tumeingia nazo mkataba na kwakweli wameanza kulipa na tunaendelea kuwahimiza wafanye hivyo ili wasije kukosa huduma ya umeme.” Alisema Mhandisi Nangali.

Aidha alisema taasisi binafsi zinadaiwa shilingi Bilioni 1 na nyingi kati ya hizo hazijaingia mkataba wa malipo ya madeni yake na TANESCO kwa hivyo akatahadharisha kuwa TANESCO haitasita kuchukua hatua za kusitisha huduma ya umeme na kwa kuonyesha kuwa Shirika halifanyi mzaha, leo hii kampuni mbili moja ikimilikiwa na mfanyabiashara maarufu Fida Hussein iliyoko Vingunguti wilayani humo imesitishiwa huduma ya umeme kufuatia deni la shilingi Milioni 29.

Kampuni nyingine iliyoonja joto ya jiwe ni Iprint iliyoko eneo la Banda la Ngozi kandokando ya barabara ya Nyerere, kampuni hiyo hadi kufikia leo Mei 4, 2017 ilikuwa ikidaiwa jumla ya shilingi Milioni 16,95.
Maafisa wa TANESCO waliokuwa kwenye operesheni ya “kukata” umeme kwa wadaiwa sugu, walikuwa na stakabadhi zinazoonyesha kuwa kufikia leo Mei 4, 2017 kampuni hizo mbili zikikuwa zikidaiwa madeni hayo.  

 Mfanyakazi wa TANESCO kivaa gloves tayari kukata umeme
 Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Afisa kutoka idara ya fedha TANESCO makao makuu, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mei 4, 2017.
 Mhandisi wa kudhibiti mapato TANESCO mkoa wa Ilala, Daniel Kimaro, akizungumza na waandishi baada ya kusitisha huduma ya umeme kwenye kampuni ya Iprint.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...