Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) kwa kushirikiana na ActionAid Tanzania waliandaa mafunzo ya siku tatu kwa wanachama wa chama cha walimu na asasi za kiraia za elimu mkoa wa Singida kuhamasisha upatikanaji wa haki za mtoto shuleni na maendeleo ya sekta ya elimu kwa kushawishi serikali kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kutumia rasilimali za ndani. 

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja Mradi kutoka ActionAid Tanzania Karoli Kadeghe alielezea katika bajeti ya elimu 2016/17, takribani bilioni 277 sawa na asilimia 31% ilitarajiwa kukusanywa kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo. 

Hata hivyo, hadi kufikia mwezi Machi 2017, wahisani walikuwa wametoa kiasi cha shilingi bilioni 132 tu sawa na asilimia 47.6%. Alisisitiza kuwa ni vyema serikali iimarishe  vyanzo vyake vya mapato vya ndani ili kuepuka aibu hii na sisi wadau wa elimu tunalo jukumu la kuisimamia serikali katika kutimiza wajibu wake. 

Kila mtu akilipa kodi stahiki kadiri ya kile anachozalisha na pia serikali ikidhibiti mianya ya upotevu wa kodi, hata kodi ya PAYE itapungua na kumpa mwalimu ahueni katika makato hayo.
 Mkufunzi wa Mafunzo, Wakili Dominic Ndunguru akielezea kuhusu ripoti ya utafiti ya shirikisho la dini (Interfaith standing committee) iliyozinduliwa Mwezi Mei mwaka 2017 kwa kuwashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi na Fedha inaliyoonyesha kuwa Tanzania kwa sasa inapoteza takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi.
  Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akiwasilisha mada kuhusu mtazamo wa upatikanaji wa elimu nchini Tanzania wakati wa Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi za Kiraia waliokutana mkoani Singida yaliyofanyika kwa siku tatu.
 Mdau wa Elimu kutoka asasi za kiraia, Lucy Mkosamali akichangia mada ya umuhimu wa uwekezaji katika maendeleo ya sekta ya elimu kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...