Katika msimu huu wa mahindi na mpunga, wakulima wengi nchini wamekua wakipokea elimu ya lishe ya mimea bure kutoka kampuni ya Yara Tanzania. Kampuni ya Yara inajiweka karibu na wakulima nchini ili kuweza kuhakikisha wanapata elimu bora ya mazao.

Akizungumzia hilo jijini Dar es salaam, Meneja Masoko wa Kampuni ya Yara Tanzania, Linda Byaba alisema kuwa Kampuni yao imeajiri Maafisa Ugani 22 wa kudumu na 37 wa muda mfupi, lengo likiwa ni kumfikishia elimu mkulima na kumuwezesha kulima kilimo cha kibiashara na sio kwa ajili ya chakula tu.

"Kampuni yetu imeajiari maafisa ugani 22 wale wa kudumu na 37 wale wa muda mfupi, tukiwa na lengo la kumfikishia elimu mkulima na kumuwezesha kulima kilimo cha kibiashara na sio kwa ajili ya chakula tu. Tukiongelea kwenye kipindi kifupi cha miezi mitatu ya kampeni zetu za mahindi zinazoendelea kaskazini  mwa nchi, wakulima zaidi ya 8,000 wameelimika kwa njia ya mashamba darasa na maafisa ugani wetu wanaowatembelea mashambani. " asema Linda Byaba.
Afisa ugani kampuni ya Yara Tanzania, Andrew Mwangomile akitoa elimu ya mbolea kwenye mahindi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mahindi.

Aidan Lunyungu kutokea Mafinga, ni mmoja wa wakulima wa mahindi alienufaika kupitia mpangilio wa lishe hiyo ya mimea. Moja ya mafanikio yake ni ongezeko la mavuno kutoka gunia 7 hadi 38 kwa ekari.  

Akizungumza wakati wa mafunzo kwa wakuliwa wenzake alisema "Mbolea hizi za kampuni ya Yara zimeninufaisha kwa mengi, kwanza unalima eneo dogo ila sasa mazao mengi na kipato kikubwa. Nilitamani sana kununua pikipiki kwa ajili ya biashara ila kupitia kipato nilichopata nimenunua pikipiki na kukarabati nyumba yangu" asema Aidan

Ushauri wa mbolea za Yara za mahindi ni kama ifuatavyo

-Baada ya kuota - Weka kifuniko kimoja cha mbolea ya YaraMila CEREAL
-Majani yakiwa 6 hadi 8 - weka kifuniko kingine kimoja cha Yara Mila CEREAL
- kabla ya Mbelewele,  weka kifuniko kingine kimoja cha mbolea hiyo hiyo ya YaraMila CEREAL

Jifunze kwa kupiga *149*50*31# chagua namba 2 kisha namba 6. Huduma hii ni BURE
Mkulima Aidan akiwa barabarani na pikipiki aliyoinunua baada ya kupata kipako kupitia zao la mahindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...