Kumekuwa na taarifa za upotoshaji katika mitandao ya kijamii kuhusu thamani halisi ya hisa za Vodacom (VTL). Kwa mfano, ujumbe uliosambazwa tarehe 19 Aprili umedai kuwa bei ya TZS 850 kwa hisa ni mara 3.8 zaidi ya thamani halisi ya hisa hizi. 

Kufikia hapo, mwandishi alikokotoa thamani ya vitabuni ya rasilimali za kampuni, akatoa dhima (madeni), na kudai kuwa albaki ndiyo thamani halisi ya hisa za wamiliki wote wa kampuni. 

Njia hii ni potofu, na inaonyesha ni kwa kiwango gani mwandishi haelewi jinsi thamani za hisa na kampuni zinavyo kokotolewa. 

Kwa mfano, mwandishi anadai kuwa ukweli kwamba bei ya toleo ya hisa za VTL ya TZS 850, sawa na mara 3.8 ya thamani ya vitabuni ya rasilimali kujitoa dhima, ni ushahidi kuwa bei imewekwa ya juu sana. Lakini siku hiyo hiyo, bei ya hisa za Safaricom katika soko la hisa la Nairobi ilikuwa ni mara 5.8 ya thamani ya vitabuni ya rasilimali baada ya kutoa dhoma.

Hivyo kampuni yetu imeona ilitolee ufafanuzi jambo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...