Na Daudi Manongi-MAELEZO.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa mkandarasi ameanza kazi ya ujenzi wa mabomba ya usambazaji katika maeneo ya Malamba Mawili,Msigani,Mbezi Luisi,Msakuzi,Kibamba,,Kiluvya,Mloganzila na Mailimoja na atakamilisha kazi hiyo mwaka huu 2017.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe wakati akijibu hoja mbalimbalia za wabunge.

“Baada ya kukamilika kwa mradi maeneo mengi ndani ya kilomita 12 ya pembezoni mwa bomba kuu la Ruvu Juu yameanza kupata huduma ya Maji”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe.

Amesema kuwa maeneo ambayo yanapata maji kwa sasa kutoka Bomba la Ruvu Juu ni pamoja na Mlandizi na vitongoji vyake, Visiga, Misugusugu, Soga, Korogwe, Picha ya Ndege, Kwa Matiasi,Tumbi, Mailimoja, Pangani, Kiluvya, Kibamba, Mloganzila, Mbezi kwa Yusufu,Mbezi Mwisho, Kimara, Mavurunza, Baruti, Kibo, Kibangu,Tabata, Segerea, Kinyerezi na Karakata.

Aidha maeneo ambayo bado hayajaanza kupata huduma ya maji yatapata huduma hiyo baada ya utekelezaji wa miradi mipya ya kujenga mtambo wa mabomba ya kusambaza maji katika maeneo yote ambayo hayana huduma hiyo, Amesema kuwa miradi hii itatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...