Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

KAMATI ya Mashindano ya Mei Mosi ,imeonya timu za Mashirika kutumia wanamichezo wasio watumishi (Watumishi Bandia ) katika mashindano hayo huku ikitangaza kutoa adhabu kali kwa taasisi ama mashirika yatakayobainika kuwatumia wachezaji hao.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo ambayo hufanyika katikamkoa ambao siku kuu ya Wanyakazi Duniani hufanyika kitaifa, timu zitakazo bainika kufanya udanganyifu zitafikwa na rungu la kufungiwa mwaka mmoja kutoshiriki mashindano hayo pamoja na faini ya kiasi cha sh 500,000.

Mbali na adhabu hiyo kwa timu iliyofanya udanganyifu ,pia viongoz wa timu husika watafungiwa kwa muda wa miaka miwili kushiriki mashindano ya Mei mosi ,adhabu itakayoenda sambamba na nakala ya barua kwa waajili wa viongozi hao ya kuonesha namna watumishi hao si waaminifu.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Mashindano hayo yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCu) baada ya kuzinduliwa jana ,Hawad Safari alisema ili kutoa uhakiki kamati imetoa maelekezo kwa wanamichezo wafike na vitamburisho vya kazi,Fomu inayoonesha mshahara pamoja na kadi ya bima ya afya.

Alisema mashindano hayo yanahusisha timu kutoka katika mashirikisho manne ambayo ni Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Uma (SHIMUTA),Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI ) ,BAMATA na Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA).
Mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa mashindano hayo ,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akitoa hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Mwamuzi wa Kike ,Salma akimtamburisha Mkuu wa wilaya timu mbalimbali zilizopo pamoja na kumkaribisha kwa ajili ya ukaguzi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa timu ya RAS Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa timu ya Geita Gold Mining.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...