Kampuni inayojishughukisha na kilimo cha Mpunga ijulikanayo kwa jina la  Highland Estates iliyopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya imepewa agizo na Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha kilichoko mkoa wa Mbeya kuwa ndani ya mwezi mmoja wahakikikishe wamesafisha mifereji yote inayozunguka ndani ya shamba lao  kwa kujenga upya miundombinu inayopoteza maji ,  kung'oa magugu maji na nyasi zote zilizoota katika mifereji ya matoleo ya maji ndani ya shamba hilo  kwani inazuia maji kupita kwa urahisi kuelekea Mto ruaha kama inavyotakiwa. Pia wametakiwa kuanza taratibu za kupatiwa cheti cha ukaguzi wa athari za mazingira kitoka Baraza lau Usimamizi wa mazingira (NEMC).

Akiongea katika ziara hiyo Mwenyekiti wa kikosi kazi hiko  Bwana Richard Muyungi alisema Uongozi wa shamba hilo wafanye juhudi za ziada kutunza mazingira yote yanayozunguka shamba hilo na kuhakikisha maji yanapita kwa urahisi katika mifereji ya matoleo ya kupeleka maji mto Ruaha Mkuu. "Tunawapa mwezi mmoja  mfanye ukarabati na mrekebishe hali ya usafi katika mifereji  ya shamba lenu baada ya muda huo tutarudi kwa ajili ya kukagua." Alisema Muyungi

Kikosi kazi hiko pia kilitembelea katika shamba la Mwekezaji lililopo wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya lijulikanalo kama Kapunga Rice Project. Kikosi kiliona matumizi mabaya ya maji kwa  kuyachepusha bila vibali  kunakofanywa na Wananchi walio maeneo ya jirani. Badala  ya mifereji ya maji iliyopo shambani hapo kurudisha maji  mto  Ruaha Mkuu. 

Maeneo mengi ya  mifereji ya kutolea maji katika shamba hilo na kupeleka mtoni yamezibwa kwa viroba na udongo ili maji yasiende mto Ruaha. Kikosi kazi kilielekeza  Kamuni michepusho yote ya maji ifungwe mara moja na Kampuni isimamie na kugharamia shughuli hiyo.  Maagizo hayo yote yametakiwa kukamilika mpaka siku ya jumanne ya tarehe 25 Aprili 2017.

Kikosi kazi hiko cha Kitaifa kilichopo Mkoani Mbeya bado kipo katika ziara ya kutembelea sehemu mbalimbali ili kujua, kufahamu, kuona na kupata maoni mbalimbali ya Wananchi ni nini haswa kinachosababisha maji kutokuingia katika mto Ruaha ili kutoa suluhisho la kudumu.


  Mfereji wa kutolea maji  kupeleka mto Ruaha Mkuu ulioko ndani ya Shamba la Mpunga la Kapunga ukiwa umejengewa tuta ili kutopitisha maji hayo kuelkea mto Ruaha kama inavyotakiwa
Magugu na nyasi zikionekana katika mfereji wa kupitishia maji  katika shamba la Mbarali ambapo magugu hayo huzuia  maji  kutopita kwa urahisi.
Mwenyekiti wa kikosi kazi cha Kitaiaf cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha  Bwana Ricahrd Muyungi akitoa maelekezo na maagizo kwa Wamiliki wa mashamba ya mpunga ya Highland Estates juu ya wanachotakiwa kufanya baada ya shamba alo kukutwa chafu sana na mifereji yao yote imejaa magugu maji.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...