Leo ni siku ya kuzaliwa Sensei Rumadha Fundi (Romi) ambaye ni Mtanzania mtaalam na mwalimu wa ngazi za kimataifa  wa karate na Yoga. 
Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi hatuwezi kulikwepa
Mtanzania huyu makazi yake ni nchini marekani. Kabla ya kujikita huko yeye  alikuwa ni mmoja ya wanafunzi wa karate katika dojo lililopo shule ya Sekondari ya wasichana ya  Zanakaki jijini Dar es salaam  chini ya mwalimu wake Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP). Baada ya hapo Sensei Rumadha akaenda kwa mafunzo zaidi nchini Japan,Sweden na Denmark. Pia akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga,
Kwa vipaji hivi vya Karate na Yoga vya ngazi ya kimataifa, Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji .Sensei Rumadha Fundi ni mwalimu wa karate na yoga 
mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana,tena mwenye nidhamu.
Sensei Rumadha ni  mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii  ughaibuni.  
Sensei Rumadha ana mkanda mweusi ngazi ya tatu (Black belt 3rd Dan ya mtindo wa Goju Ryu, ambayo ni chimbuko la  dojo iliyojengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha, Okinawa baada ya  kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu , Master Chijun  Miyagi , ambayo hivi sasa  inaendeshwa na mtoto wake Yoshihiro Kancho Miyazato. Sensei Rumadha Fundi, kwa sasa ndiye  mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" tawi la Tanzania. 
Pichani wa nne kushoto waliosimama ni Sensei Rumadha akiwa nchininUreno akishiriki katika kongamano la Karate la kimataifa la " European Jundokan  Gasshuku 2016" mwaka jana akiwa mjumbe wa  kitengo kinachosimamia ubora na uthabiti wa  sanaa asili ya mitindo ya  karate toka Okinawa kiitwacho " OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION" ambacho kimefanya mabadiliko ya kutofautisha  karate asilia na ile ya  kimichezo itayokuwa katika michezo ya  Olympiki.

Kutokana na mabadiliko ya  kimbinu na ufasaha yanayoonekana katika michezo hiyo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi  Karate asilia itavyozidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi, na pia, kuhakikisha kiundani zaidi kwamba  mbinu halisi za sanaa hiyo zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya  Karate waliopata mafunzo visiwani Okinawa duniani kote. 

Hivyo Sensei Rumadha kwa sasa ni mjumbe wa timu hiyo ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka mitindo mbalimbali inayotambulika na " BUDOKAN" kusambaza uadilifu wa mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa  inafundisha na waasisi wake asilia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...