MAKAMU wa Rais mstaafu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed  Ghalib Bilal anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kili Challenge kwa mwaka 2017, kampeni hiyo yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi ya vurusi vya Ukimwi.
Kampeni hiyo ambayo imeandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na virusi vya Ukimwi  nchini (TACAIDS).
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo, Makamu wa Rais wa mradi endelevu wa Mgodi (GGM), Simo Shayo amesema uzinduzii huo utafanyika kwenye Hyatt Kilimanjaro  Hoteli Dar es salaam.
‘’Nawakalibisha watu wote kujitokeza katika kuchangia fedha hizi ili zisaidie katika kupambana na maambuzi haya, kwani jukumu la kupambana na ugonjwa huu sio wa serikali peke yake bali hata jamii nzima inahaja ya kujitokeza na kupambana na ugonjwa huu’’Amesema Shayo.

Shayo amebainisha kuwa  katika kampeni hiyo wameshirikiana na wasanii akiwemo Mrisho  Mpoto kwa lengo la kuiamsha jamii ili ijitokeze katika kupambana na vita hiyo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa (TACAIDS)Dkt Leonard Maboko amewasihi Makampuni mengine yaige mfano  wa (GGM) Katika kuhakisha watahakikisha ugonjwa wa Ukimwi unatokomezwa nchini.
Makamu wa Rais wa miradi endelevu wa Mgodi (GGM), Simo Shayo akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo pichani) juu uzinduzi wa kampeni ya Kili Challenge kwa mwaka 2017, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko naye akizungumzia Kampeni hiyo katika mkutano ulio fanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwanamziki maarufu nchini, Mrisho Mpoto ambaye ni Balozi wa Kampeni ya Kili Challenge 2017 amewasihi wasanii wenzake kujitokeza na kuungana naye katika vita ya kupambana dhidi ya maambuki ya virusi vya Ukimwi.leo jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa (TACAIDS) na waandishi wa habari wakimsikiliza Makamu wa Rais wa miradi endelevu wa Mgodi (GGM) ,Simo Shayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...