Wafanyabiashara
watatu akiwemo raia wa Zambia mmoja wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma
za uhujumi uchumi ikiwemo kusafirisha bidhaa kwa kificho
Washtakiwa
hao ambao wamefikishwa mbele ya Mahakimu wawili tofauti ni Sultani
Ibrahimu, (36), mwarabu Mkazi wa Usalama Temeke, Augustino Kalumba (39)
raia wa Zambia na Ramadhani Hamisi maarufu kama Ukwaju (48) anaishi
Kinondoni Hananasifu.
Wanadaiwa kutenda makosa hayo kinyume na sheria ya Umoja wa nchi za Afrika Mashariki ya kudhibiti ushuru. Mbele
ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba washtakiwa Sultan Ibrahimu na
Augustino Kalumba wamesomewa mashtaka matatu, la kula njama,
kusafirisha Mali iliyofichwa na kuitia hasara serikali ya Jamuhuri wa
Muungano wa Tanzania zaidi ya shilingi milioni 287.8.
Mwendesha
mashtaka Nassoro Katuga akisaidiana na Wakili Batlida Mushi amedai kuwa
kati ya Decemba 1 mwaka jana na Machi 1 mwaka huu katika eneo
lisilojulikana washtakiwa hao wakiwa na wenzao ambao bado hawajakamatwa
walikula njama ya kusafirisha mali.
Katika shtaka la pili imedaiwa
kuwa kati ya Decemba 1 hadi 31, mwaka jana katika makao makuu ya
Bandari ya Tanzania yaliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam
washtakiwa waliingiza magari matatu ambayo ni Range Rover sports, Zenye
naomba tofauti tofauti.
Imedaiwa kuwa magari hayo yalikuwa
yamepakiwa pamoja na nguo za mitumba na viatu kwenye kontena namba MSKU
9914168 kwa nia ya kuwadanganya maafisa wa ushuru.
Aidha
washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuingiza Mali hizo wakiwa
wamezificha na kuisababishia serikali ya Tanzania kuingia hasara zaidi
ya shilingi 287.8. Mbele ya Hakimu Respiciou Mwijage washtakiwa Sultan Ibrahim na Ramadhani Hamis wamesomewa mashtaka matatu.
Imedaiwa
kuwa kati ya Decemba Mosi mwaka jana na March 4 mwaka huu jijini Dar es
Salaam, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la Kuficha Mzigo
wakati wakiuingiza nchini.
Imeendelea kudaiwa kuwa, kwa pamoja
washtakiwa hao waliingiza Mzigo wa magari matatu wakiwa wameyaficha ili
kuweza kuwaficha maafisa ushuru.
Wakili Katuga amedai kuwa kitendo
hicho kimeikosesha serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania mapato
zaidi ya shilingi milioni 190.9. Hata hivyo washtakiwa hao
hawakuruhisiwa kujibu kitu chochote na wamerudishwa rumande kwa kuwa
mashtaka dhidi yao yako chini ya sheria ya uhujumu uchumi ambayo
Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kutoa dhamana.Aidha Wakili Katuga
aliiarifu mahakama kuwa DPP bado hajatoa kibali kwa mahakama ya Kisutu
kusikiliza kesi hiyo.
Kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo Aprili 12 mwaka huu. Upelelezi bado haujakamilika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...