MKUU
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amefanikiwa kumaliza mgogoro wa muda
mrefu kati ya mwekezaji katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA)
Makao iliyopo wilayani Meatu, na baadhi ya vijiji vinavyounda jumuiya
hiyo.
Mwekezaji huyo Mwiba Holdings, amekuwa na mgogoro wa mipaka,
mkataba wa kumiliki ardhi na uanzishaji wa ranchi na baadhi ya vijiji
hivyo kiasi cha kusababisha kuwa na mahusiano mabaya na wananchi ambao
wamekuwa wakisusia misaada mbalimbali inayotolewa na mwekezaji huyo.
Hata
hivyo, chanzo halisi cha mgogoro huo kimegundulika kuwa ni viongozi wa
baadhi ya vijiji ambao wamekuwa wakipigania maslahi yao binafsi huku
wakisambaza taarifa za upotoshaji juu ya mwekezaji huyo na kujenga chuki
kwa wananchi.
Vijiji
vinavyounda WMA ya Makao ni pamoja na Makao, Iramba ndogo, Sapa,
Mwangudo, Jinamo, Lukale, Mbushi, Mwabagimu na Sunga. Baadhi ya viongozi
hao wa vijiji pia wamekuwa wakisambaza taarifa potofu kwa wananchi
kwamba Mkuu huyo wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Meatu wamehongwa na
mwekezaji ili kuwakandamiza wananchi, jambo lililothibitika kuwa si la
kweli.
Mkuu wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi baina ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Dk Titus Kamani akizungumza katika
kikao cha usuluhishi baina ya wananchi wa Meatu na Mwekezaji wa Mwiba
Holdings kilichofanyika mjini Mwanhuzi mwishoni mwa wiaki.
Mkuu wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi
baina ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu
kilichofanyika mwishoni mwa wiki
Kuhusu
mgogoro wa mpaka hasa katika kijiji cha Buhongoja ambako alama ya mpaka
yenye namba 314 inadaiwa kusogezwa kinyemela kwa umbali wa kilomita 10,
Mkuu huyo wa mkoa alizitaka pande zinazohusika kukutana na kutatua
tatizo hilo kwa kurejea katika eneo la awali bila ya mikwaruzano yoyote.
Aliamuru pia pande zinazohusika katika suala la mkataba wa umiliki wa
ardhi,kukaa meza moja na kuacha mambo ya kukimbilia kwa wasuluhishi
ambao wamekuwa wakidai fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwa
maendeleo ya vijiji au wilaya ya Meatu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...